Na Penina Malundo,Timesmajira
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) inatarajia kuzindua mfumo wa kidigitali wa utatuzi wa Malalamiko ya wananchi(FCRS), utakaomwezesha mtumiaji wa huduma za kifedha kuwasilisha malalamiko kutumia mtandao, kuanzia Januari mwaka 2025.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam, jana, na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma Jumuishi za Fedha wa BoT, Nangi Massawe akifungua warsha ya siku mbili kuhusu mfumo wa malalamiko kwa wawakilishi wa taasisi za fedha nchini.
Amesema mfumo huo tayari umekamilika na kinachofanyika sasa ni kutoa elimu kwa taasisi za fedha kuelewa kwani wao ndio wanaokutana na wateja.
Amesema jukumu kubwa la benki kuu ni kuhakikisha linamlinda mtumiaji wa huduma za kifedha kuwa na uelewa wa masuala ya kifedha, kujua ni wapi atawasilisha malalamiko yake na kupata haki, kani wamekuwa wakifanya hivyo kujenga imani na huduma za kifedha na kutumia huduma rasmi kukamilisha lengo la kuwepo kwa huduma jumuishi.
Naye Kaimu Meneja wa Kumlinda mtumiaji wa Huduma za Kifedha, Dk. Hadija Kishimba,
amesema lengo la BoT, kuandaa warsha hiyo kwa taasisi za fedha ni kuuelewa mfumo, kwani wao ndiyo wanaokutana na wateja.
Amewataka watumie mfumo huo kwa sababu unakwenda kusogeza huduma kwa mwananchi kwani wanataka alalamike kupitia mtandao kwa njia ya kompyuta.
Amesema lengo la BoT, ni kutafuta namna bora ya kutumia teknolojia kuwafikia wananchi katika kuwapa huduma, kwani jukumu la benki hiyo ni kuongeza fedha jumuishi nchini, hvyo kumekuwa na changamoto ya kuongeza imani mtu akipata tatizo apate ufumbuzi wa haraka.
Amesema kwa sasa wanapokea malalamiko kupitia matawi yao na dawati ya malamiko kupitia njia ya barua pepe, simu au kuandika barua na kufikisha hivyo, waona njia hiyo inaweza kutowafikisha zaidi ya teknolojia.
Kwa upande wake, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa bebki ya NMB, Elizabeth Mhina amesema wamefurahi BoT kuweka mfumo kuwa wa moja kwa moja hivyo itawasaidia kurahisisha kazi na kuwafikia wateja na Watanzania kwa ujumla.
“Yapo malalamiko mengi wamekuwa wakiyapokea kikubwa ni changamoto ya elimu kwa wateja kwa mfano kuibiwa fedha katika ATM na kadi wamekuwa wakiyapata kila siku, ni suala la elimu kuwa wasitoe namba za siri, bado tunatoa elimu kuwafikia wateja wetu kudhibiti wizi,” amesema.
More Stories
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais
NIDA yawakumbusha wananchi kuchukua vitambulisho vyao