January 13, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bondia Mcgregor akubali kichapo dhidi ya Poirter

LAS VEGAS, Marekani

BONDIA Conor mcgregor amekubali kichapo tena dhidi ya Dustin Poirter, baada ya kupigwa kwa mara ya pili mfululizo katika pambano la UFC 264, lililopigwa usiku wa kuamkia leo mjini Las Vegas Marekani.

Hata hivyo haikuwa rahisi kwa Dustin kumchapa Conor kwa TKO baada ya raundi ya kwanza bila ya bondia huyo anayetajwa kama mwanamichezo anayevuta mkwanja mrefu zaidi duniani kuvunjika mguu.

Pambano hilo lilisimamishwa na madaktari wa ulingoni hapo, kufuatia kuona Conor asingeweza kuendelea na pambano hilo, na hivyo kumpa Poirter ushindi wa pili mfululizo dhidi yake.

Pamoja na kupigwa na kuvunja mguu, Conor mwenye umri wa miaka 32, amesema vita kati yake na Dustin Poirier haijaisha.

Conor alimpiga Poirter kwa TKO ya raundi ya kwanza katika UFC 178 mwaka 2014, lakini Poirter alilipa kisasi kwa kumchapa Conor kwa TKO ya raundi ya pili katika UFC 257 Januari mwaka huu, kabla ya usiku wa kuamkia leo bondia huyo kushinda tena.