December 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bondia Foreman amuonya Tyson kupigana na Jones

LOS ANGELES, Marekani

BONDIA George Foreman amemuonya Bondia mkongwe Mike Tyson kurejea kwenye mchezo wa ngumi, huku akitarajiwa kupanda ulingo dhidi ya Roy Jones Jr mpambanao utakaofanyika Los Angeles, nchini Marekani.

Tyson, mwenye umri wa miaka 54 raia wa Marekani, hajapigana ngumi za ushindani tangu aliposhindwa dhidi ya Kevin McBride mnamo 2005 huko Washington.

Hata hivyo Jones Jr mepitwa miaka mitatu na Tyson pamoja na George Foreman, bingwa wa zamani wa uzito wa juu mara mbili, anaamini hapaswi kujiweka katika nafasi kama hiyo.

Foreman amesema, Kwa sasa Tyson hapaswi kurejea kwenye mchezo wa ngumi kwa umri umeshamtupa mkono, hivyo ni mbaya sana kupanda ulingoni na kijana aliyemzidi umri wa miaka mitatu ukizingatia kwa muda mrefu nguli huyo hajapigana.

“Huo utakuwa kama uwendawazimu wa muda mfupi. Ninafananisha na kijana ambaye anataka kupanda kwenye mashua na kwenda baharini. Halafu yeye hutaka kutoka nje na mawimbi makubwa yanaanza kuja baharini na upepo unavuma na anajiuliza, “Bwana, kwa nini nimewahi kufanya hivi?,” alisema Foreman.

Hata hivyo Foreman alisema, Tyson anatamani sana kupigana tena. Maana kuna hisia zinawasumbua mabondia wote waliostaafu bila kujali umri wao.

Foreman mwenyewe hakupigana kwa miaka kumi kati ya umri wa miaka 28 na 38 ingawa hiyo haikuwa kali kama Tyson kurejea kupigana akiwa na 54.