November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bona Cup kushindania milioni tano

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Segerea

Mashindano ya kugombea Kombe la Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah CUP 2022 yanatarajia kuanza Desemba mwaka huu ambapo jumla ya timu 64 zitashiriki .

Akizungumza na waandishi wa habari Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli, alisema mashindano hayo yanashirikisha timu 64 za Jimbo la Segerea kwa ajili ya kutafuta vipaji kwa Vijana.

“Chama Cha Mapinduzi CCM kinaimiza Michezo mashindano ya Bonah cup yanatarajia kumalizika January 18 kwa Sasa ni hatua ya mtoano katika timu 64 ” alisema Bonah .

Mbunge Bonah amewakaribisha Wadau mbalimbali katika sekta ya Michezo kuangalia vipaji katika mashindano hayo .

Mbunge Bonah alitaja zawadi za mashindano hayo ambapo mshindi wa kwanza anatarajia kupata milioni 5 mshindi wa pili milioni tatu na mshindi wa tatu milioni 2 .

Alisema vijana wengi wapo mitaani hivyo kuanzisha kwa mashindano hayo ya mpira miguu ni fursa kwa vijana wengi waweze kushiriki ambao mitaani kwani Michezo ni ajira pia ujenga Afya .

Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Segerea Lutta Rucharaba alisema mashindano hayo yatafanyika katika Viwanja vinane tofauti ambavyo vipo jimbo la Segerea kikiwemo Segerea ,Tabata ,Yombo ,Buguruni ,Vingunguti ,Kimanga ,Bonyokwa ,Stakishari na Sukita .

Katibu wa Mbunge alisema kanuni za mashindano hayo wachezaji lazima wawe Wakazi wa Jimbo la SEGEREA timu ikileta mchezaji kutoka nje ya SEGEREA au mchezaji wa Ligi kuu inakuwa imejiondoa katika mashindano hayo ya kisiasa ambapo wamuzi wake kutoka shirikisho la mpira miguu Tanzania DRFA .

Alisema mashindano hayo kingilio Bure yatakuwa yanasimamiwa na Kamati mbalimbali wakiwemo Wenyeviti wa Serikali za Mitaa makatibu Kata na Umoja wa Vijana wa kila Kata .