December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), hiyo,Godfred Mbanyi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).

Bodi ya Watalaam wa Ununuzi yatangaza matokeo mtihani

Na Penina Malundo

BODI ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetangaza matokeo ya mitihani ya 19 iliyofanyika nchini mwaka jana huku watahiniwa 602 sawa na asilimia 56.4 wakifaulu mtihani huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo,Godfred Mbanyi amesema jumla ya watahiniwa 1,196 ndio waliosajiliwa kufanya mitihani huo, lakini waliofanikiwa kufanya mitihani hiyo ni watahiniwa 1,067.

Amesema licha ya asilimia 56.4 ya watahiniwa wote waolifaulu,watahiniwa 441 sawa na asilimia 41.3 wamefeli baadhi ya masomo hivyo wanaruhusiwa kurudia tena mitihani hiyo.

“Watahiniwa 24 sawa na asilimia 2.3 hawa wamefeli kabisa masomo ya ngazi zote ila watahiniwa watatu waliofanya mitihani walifanya vizuri katika ngazi ya professional stage I ,II na masomo ya utafiti,” amesema na kuongeza;

“Pia katika mitihani hiyo wanafunzi 10 wamefutiwa haki ya kurudia mitihani kutokana na kurudia mara tatu na kushindwa kufanya vizuri hivyo wanapaswa kuanza mchakato upya wa kujisajili ili kuweza kufanya mitihani,” amesema

Aidha amesema baada ya kufanya uchunguzi waligundua watahiniwa hao walifeli mitihani kutokana na kutomaliza mitahala ya mafunzo, maandalizi hafifu, kutokuwa na mbinu sahihi za kujibu maswali ya kitaalam ya taaluma kwa upande wa masomo ya hesabati.

“Kutokana na kuchelewa kutolewa kwa matokeo ya mitihani hiyo wanafunzi waliofeli somo moja au mawili wanaruhusiwa kujisajili kwa ajili ya mitihani ya 20 ya Bodi hiyo itakayofanyika Agosti 11 hadi 14 mwaka huu,” amesema na kuongeza;

“Dirisha la usajili litakuwa wazi kuanzi leo (jana) hadi Julai 11,mwaka huu,” amesema

Amesema licha ya kuchelewa kutoa matokeo ya 19 Bodi bado ina mpango wa kuendesha mitihani ya 21 itakayofanyika mwezi huo.

Mwishooo