May 10, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bodi ya Tume ya Ulinzi wa taarifa binafsi wazinduliwa rasmi

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

WAZIRI wa Habari,Mawasilino na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye Amezindua Bodi ya tume ya ulinzi wa taarifa binafsi huku akiwataka wajumbe wa Bodi hiyo mpya kuendeleza na kuandika historia ambayo inakwenda kutengeneza jamii ya watu wastarabu kwa kuanzishwa tume hiyo.

Akiongea leo jijini Dodoma kabla ya kuzindua Bodi hiyo Waziri huyo amesema ilianza kutungwa sheria ikazaa tume na baadaye ikazaa Bodi ambapo lengo kuu ni kuhakikisha taarifa za watu binafsi zinatunzwa.

Amesema tume hiyo mpya inajukumu la kulinda heshima, haki na utu kwa kuhakikisha taarifa za watanzania na hata wageni taarifa zao kuwa sehemu salama na zinatumika kwa kujali haki heshima na utu ili watu waone Tanzania ni taifa salama kwa huduma za kidigitali

“Tume hii ni mpya wenzetu huku mataifa mengine walishaanza na sisi hapa Tanzania Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan na ndio maana akaamua ianzishwe na amefanya kwa imani, “

Na kuongeza kusema “Wito wangu kwenu ni kuilinda imani ya Rais wetu kwani mchakato ulikuwa mkubwa kuwapata nyinyi na kuipata tume hii na ukweli kutoka moyoni ninatamani kuja kusikia tume hii ya taarifa binafsi nchini ni Bora kuliko tume nyingine duniani, ” Amesema Waziri Nnauye

Amesema matumaini ya taifa ni kuona faragha zao zinalindwa nchini kwani kuanzia sasa taarifa za watu zinakusanywa ,zinachakatwa na kutuma sehemu sahihi ambapo misingi mikuu inazingatiwa ya kikanda na kimataifa .

“Ninamatumaini baada ya muda watu watakuja kujifunza kwetu juu ya tume hii kwani nchi ya Tanzania ni mwanachama kwa nchi mbalimbali imeanza vizuri hivyo tume kuhakikisha inaanza utekelezaji wa majukumu yake kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu zilizowekwa na msikubali kuingiliwa na badala yake mlindwe na sheria msiendeshwe, ” Amesisitiza Waziri Nnauye

Na kuongeza “Utoaji wa huduma uhakikishe unaendana na huduma za kidigitali pia mifumo isomane na iwepo kila mkoa ili watu watumie mifumo kuliko watu kutoka mikoani kuja Dodoma au Dar es Salaam kutafuta mifumo nasisitiza muweke mifumo inayisomana, ” Amesema.

Kwa Upande Wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Khamis Abdullah alikuwepo wakati wa ugawaji wa vitendea kazi na mkakati huo ulikuwa unalenga mikakati mitano

Amesema hayo ni Matokeo ya siku 100 ambapo wamefanikiwa kwa asilimia 90 kwani wameweza kujenga taasisi yenye sura nzuri inaonekana kujenga utambulisho anuani pamoja na logo na wako kwenye kutengeneza mpango mkakati.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ulinzi wa Tume ya Taarifa Binafsi Balozi Mohamed Adadi Rajabu wanemshukuru kwa uteuzi wake kwa kuwaaminiwa na kuteuliwa kwenye tume hiyo na ahadi yao ni kufanya kazi kwa weledi unaotakiwa ili kuhakikisha tume inafanya kazi vile inavyotakiwa

“Kikubwa ni kuelewa sheria namba 11 inaeleza majukumu ya tume inataka nini, majukumu ya tume inawataka kutunza Siri za watu taarifa za watu binafsi zinatunzwa, ” Amesema

Na kuongeza kuwa “Lakini kupitia maaelekezo ya waziri tutafanya kazi vile atakavyoelekeza bila kusahau kutoa uelewa kwa umma ili kujua kazi na majukumu ya tume, “Amesema Mwenyekiti huyo.