October 2, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bodi ya Maji Bonde la Rufiji yajidhatiti kulinda vyanzo vya maji.

Na David John, Timesmajira Online

MKURUGENZI mkuu wa Bodi ya Maji Bonde la Rufiji Mhandisi Florence Mahay amesema kuwa bodi ya maji katika bonde la rufiji lina kazi moja tu ya kusimamia rasilimali za maji ambapo kazi hiyo wanaifanya kwa kufanya kazi kuu tatu ambazo ni kuna rasilimali maji kwa kiasi gani mfumo wa mto rufiji,kugawa maji kwa sekta zote zinazotumia maji,kutunza vyanzo vya maji na kuzuia uchafuzi wa rasilimali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 6 mwaka huu katika ofisi za Bodi ya Maji zilizopo mkoani Iringa Mkurugenzi Mahay amesema kuwa amelazimika kuwaita wandishi wahabari kwa lengo la kutoa fursa ya kushirikiana nao na hasa katika kuhabarisha jamii kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo ya maji kupitia bonde la rufiji.

Pia amesema kuwa wametoa fursa kwa waandishi kutembelea sehemu kadhaa za bonde ili kuweza kupata uelewa utakaowawezesha kutoa taarifa ambazo watakuwa wamezielewa ipasavyo na watatembelea bonde na kuona kazi zinazofanyika hasa kupitia kazi tatu ambazo amezitaja ambapo kwao fursa nzuri kwa wanahabari hao kuweza kuhabarisha umma juu ya kazi zinazoendelea.

Akizungumzia kuhusu kuhifadhi vyanzo vya maji Mhandisi Mahay Amesema serikali imewekeza katika bonde la rufiji kwa kujenga miundombinu hasa katika uzalishaji wa umeme na miundombinu mitatu ambayo imeshajengwa na inafanya kazi ni ikiwamo Bwawa la Mtera,Kidatu na kihansi kote tayari kumeshajengwa na kuna fanyakazi na yote ipo katika bonde la rufiji.

Ameongeza kuwa kwa sasa kuna mradi mkubwa wa Bwawa la Julius Nyerere ambao ujenzi wake unaendelea hivyo lazima umma ujuwe kwamba kazi ya kutunza vyanzo vya maji ,kulinda mtiririko wa maji kwenye mito wanaendelea kuifanya ili kuhakikisha kwamba Bwawa la Julius Nyerere linajaa na kazi ya kuzalisha umeme itaendelea.

Amefafanua kuwa kukamilika kwa Bwawa hilo kutawezesha kufaidisha uchumi wa nchi “Bonde lina umuhimu mkubwa sana kwa uchumi wa nchi ikiwamo usalama wa chakula na karibu asilimia hamsini ya miradi yote ya umwagiliaji ipo katika bonde hili na asilimia thamanini ya miradi ya kuzalisha umeme wa maji ipo katika bonde hili lakini kuna mbuga za wanyama karibu sita zote zipo katika bonde hili” amesema Mhandisi Mahay

Nakuongeza kuwa “Bonde hilo ni muhimu sana kwa maendeleo ya kiuchumi ya taifa na kuna vidakio vitatu ambavyo ni kilombero,Great Ruaha,Ruweb lakini katika kidakio cha Great Ruaha kumejaa na hakuna maji kwaajili ya miradi mipya lakini kungine kwa hali ilivyo maji yapo na mfumo wa rufiji unaweza kuzalisha mita za ujazo Bilioni 40 kwa maana bilioni 31 juu ya ardhi na bilioni 9 ni chini ya ardhi kwahiyo maji yapo

Amesema kuhusu vibari walivyotoa kwa matumizi ya maji yanayotumiwa ni bilioni 2.4 kwahiyo maji yapo lakini katika maji bilini 2.4 asilimia tisini yapo kwenye bonde la Great Ruaha.

Pia mkurugenzi Mahay amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kauli aliyoitoa Disemba 22 mwaka jana wakati akizindua ujazaji wa Maji bwawa la Julius Nyerere alitoa maelekezo na maagizo kwamba Bodi isiendelee kutoa vibari kwa matumizi ya miradi mikubwa inayoenda kutekelezwa na bodi kupitia kikao chake ilishasitisha utoaji wa vibari kuazia mwezi wa kwanza mpaka pale ujazaji wa maji bwawa hilo litakapokalimika.

Mhandisi Mahay amesema kuwa kwa watu ambao wanatumia maji bila vibari sheria ipo na kwa wale wakubwa tayari hatua zimeaza kuchukuliwa na kuhakikisha kwamba hawatumii tena maji hayo na badala yake kuweza kuruhu mtiririko wa maji kwenye mto rufiji

“Wito wangu kwa watumia maji wote wafuate utaratibu wa kupata vibari wakati wa kutumia maji na mtu asiazishe mradi bila kuwasiliana na bodi na kuwa na uhakika wa kwamba maji yapo hivyo nivema wakafuata utaratibu na kuhusu kutuza vyanzo vya maji tunafanya hivi ili kuhakikisha mtiririko wa maji unakuwa endelevu na ndio maana tunafanya kazi na jumuiya za watumia maji ili kuhakikisha maji yanalindwa.”amesema Mahay

Kwa uapande wake Mhandisi Ally Diwani msimamizi wa kitengo cha Mhaidrolojia Bodi ya maji bonde la rufiji iringa amesema kuwa yeye anasimamia kitengo cha kufanya tathimini ya maji kwenye bonde ambapo kitengo hicjo ndio kinatoa maji ya kiasi gani cha maji kilichopo kwenye bonde la mto rufiji

Amesema kuwa kingo hicho kina vituo 137 na vituo 59 ni vya kupima mtiririko wa maji juu ya ardhi na vituo 29 ni vya kupima miririko wa maji chini ya ardhi na vituo 49 ni vya kupima hali ya hewa kwa maana kuchukua takwimu na vituo hivyo vyote vipo katika maeneo mbalimbali kwenye bonde na kuhusu vituo hivyo kwenye bonde ndio vinaleta majibu ya kiasi cha maji kilichopo.

Amesema kuwa kupitia vituo hivyo ni kwamba kwenye upande wa juu ya ardhi kuna kiasi cha maji bilioni 31 na chini ya maji bilioni 9 na katika kufanya tathimini ya maji yaliyopo kwenye bonde la rufiji wanaendelea vizuri kwa maana ya usimamizi lakini changamoto zipo ndogo ndogo ambazo ni uharibifu kwa maana ya ulinzi na uvunjaji wa vifaa vinavyosaidia kwenye eneo la upimaji.

Naye Mhandisi wa Rasilimali za maji kwenye Bonde la mto rufiji Gallusi Ndunguru amesema kuwa yeye anasimamia kitengo cha ugawaji wa rasiliamali za maji na katika kitengo hicho kinafanya kazi ya kugawa maji kwa njia ya vibari na kwasababu rasilimali za maji ni adimu na zinapungua hivyo lazima pawepo na utatibu wa maji yaliyopo

Amesema mtu yeyote anataka kuchukua maji lazima iwe kwenye kisima au kungineko lazima awe na kibari kutoka bodi ya maji na utaratibu ni kwamba anajaza fomu na baada ya hapo ombi lake linatangazwa kwenye gazeti la serikali kwa siku arobaini na pia linapita kwa bodi.

Amesema hasi sasa wametoa vibari 2005 na vinari kumi kwa ajili ya kutiririsha maji taka na kwa upande wa maombi yanakuja kwa awamu lakini wakati mungine wanalazimika kukataa maombi hayo pindi wanapoona maji hayajitoshelezi kwa matumizi mengine isipokuwa kwa matumizi ya binadamu.