December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bodaboda Mwananyamala ashinda Milioni 10 za BIKO

Mwandishi Wetu, TimesMajira Online Dar

DEREVA wa bodaboda Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, Rashid Ally Handiko, amefanikiwa kushinda Sh Milioni 10 za bahati nasibu ya Watanzania Biko kwa kupitia droo yake kubwa iliyofanyika mwishoni mwa wiki,ikiwa ni mwendelezo wa watu wengi kuendelea kushinda mamilioni ya zawadi kutoka kwenye bahati nasibu hiyo.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Ally alisema amefarijika kuona ameshinda fedha sanjari na kukabidhiwa kwa haraka kiasi cha kuamua kitu cha kuzifanyia kwa ajili ya kuendeleza maisha yake.

“Nashukuru kufanikiwa kushinda fedha zangu na kukabidhiwa bank kwa haraka kwa maana ndio njia ya kuzipatia kazi ya kufanya, ukizingatia kuwa hii njia nzuri ya kukuza uchumi wangu,” Alisema Ally.

Mbali na wanaocheza kwa kupitia www.biko.co.tz, pia wanaotumia simu za kawaida nao wataendelea kucheza kama zamani kwa kutumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456 na wote kujishindia kuanzia sh 2500 hadi milioni tano papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa zinazofanyika kila Jumapili.

Kianzio cha kucheza Biko ni sh 1000 na kuendelea ambapo Watanzania wengi wameendelea kushinda zawadi za papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa za kushinda hadi sh milioni 40, zikiwa na lengo la kuboresha maisha ya wote wanaocheza Biko.

Droo za biko zinafanyika kila Jumapili ambapo Watanzania wengi wamekuwa wakishinda zawadi kubwa za wiki bila kusahau papo kwa hapo zinazoingia moja kwa moja kwenye simu za mkononi.

Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja kushoto akimkabidhi fedha zake Rrashid Ally Sh Milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye droo kubwa iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki. Kulia ni Meneja Uhusiano wa bank ya CRDB Tawi la Palm Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha wetu.
Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja, akiwa mwenye furaha kubwa baada ya kufanikiwa kumkabidhi Rashid Ally fedha zake Sh Milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye droo kubwa ya Biko. Picha na Mpiga picha wetu.