Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
BARAZA la Michezo Tanzania(BMT)limesema Serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa viwanja vya michezo ambapo ujenzi wa uwanja mpya wa michezo Dodoma unaotarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni utagharimu shilingi Bilioni 310.
Hayo yamebainishwa leo,Februari 18,2025 na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Neema Msitha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo na muelekeo wa baraza hilo kwa kipindi cha miaka miaka 4 ya uongozi wa Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Akizungumzia maendeleo na mafanikio kupitia baraza hilo Neema ameeleza kuwa ujenzi wa uwanja mpya wa michezo Arusha utagharimu shilingi Bilioni 338 hadi kukamilika kwake.

Vilevile amesema serikali imetumia kiasi cha shilingi bilioni 31 kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa uwanja wa Benjamin Mkapa kwa lengo ya uboreshaji wa sekta ya michezo.
“Viwanja vingine vya michezo ni pamoja na viwanja vya mazoezi ikiwemo Gymkhana, Leaders Club,TIRDO, Law School na uwanja wa Farasi hadi kukamilika vitatumia shilingi Bilioni 21,”amesema.
Mafanikio mengine yaliyoyabainisha kwa kipindi cha miaka 4 ya uongozi wa Rais Samia ni pamoja na Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa Kanda ya nne wa kupinga dawa na mbinu haramu michezoni uliofanyika Dar es Salaam mwezi Novemba 2024.
Akielezea mafanikio amesema kuwa katika kuwashawishi wawekezaji katika ujenzi wa viwanja vya michezo,Serikali imeondoa kodi ya nyasi bandia, hali iliyosaidia uwepo wa viwanja katika ngazi za Halmshauri na kusaidia vijana wengi kushiriki katika michezo.
“Katika kukuza michezo nchini Serikali ya Tanzania imefanikiwa kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Michezo wenye jukumu la kuwezesha timu za Taifa, kutoa mafunzo kwa wataalamu wa michezo, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya michezo, kununua vifaa vya michezo na kuendeleza vipaji”amesema Msitha.
More Stories
Serikali ,Washirika wa Maendeleo waweka mkakati utekelezaji Dira ya 2050
Dkt.Mpango aipongeza STAMICO kuwa mfano bora utekelezaji matumizi nishati safi ya kupikia
Wezi wa mapato manispaa Tabora kukiona cha moto