NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA
MFUKO
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umewakumbusha wanachama wake
kuwa, huduma zote zinazohusiana na uanachama wa mwanachama zinapatikana mtandaoni,
(PSSSF Kiganjani).
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko (wapili kulia), akimsikiliza Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Lulu Mengele alipotembelea banda la Mfuko huo, kwenye Maonesho ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA), katika uwanja wa General Tyre, Njiro jijini Arusha, Aprili 28, 2024.
NSSF, inashiriki katika maonesho hayo ili kutoa fursa kwa wananchi kuweza kupata taarifa kuhusu shughuli zinazotekelezwa na Mfuko huo. Maonesho ya mwaka huu 2024, yamebeba kauli mbiu isemayo, “Athari za mabadiliko ya tabia nchi katika usalama na afya kazini; Sajili eneo la kazi OSHA katika harakati za kupunguza athari hizo.”
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko (katikati), akizungumza jambo wakati alipotembelea banda la NSSF, kwenye Maonesho ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA), katika uwanja wa General Tyre, Njiro jijini Arusha, Aprili 28, 2024. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisis ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas Katambi, Mkurugenzi Mkuu, OSHA, Khadija Mwenda (wapili kushoto).
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua