January 1, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Biteko ashiriki ibada kuaga mwili wa Askofu Kweka(HABARI PICHA)

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akizungumza  na  Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini,  Dkt. Fredrick Onaeli Shoo kabla ya Ibada ya maalum ya kuaga mwili wa Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Erasto Kweka katika Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro leo.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia Kifo cha Baba Askofu Mstaafu Dkt. Erasto Kweka, wakati wa Ibada maalumu ya kuaga mwili leo Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro. Kulia kwake ni Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Fredrick Onaeli Shoo.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akitoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Erasto Kweka, kabla ya ibada maalum ya kuaga mwili wa Baba Askofu leo Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.
Familia ya Marehemu Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Erasto Kweka na waombolezaji mbalimbali wakiwa katika Kanisa la Usharika wa Moshi Mjini kabla ya ibada maalum ya kuaga mwili wa Baba Askofu leo.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko Akiaga Mwili wa Marehemu Baba Askofu Mstaafu Dkt. Erasto Kweka, wakati wa ibada maalum ya kuaga mwili leo, Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.