May 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TCAA yaibuka mshindi wa pili,Tuzo mwajiri Bora

Na Penina Malundo

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imeibuka kuwa mshindi wa pili katika upande wa taasisi za umma kwenye kinyang’anyiro cha Tuzo za Mwajiri Bora kwa mwaka 2023 iliyoandaliwa na Chama cha waajiri Tanzania (ATE).

Akizungumza Jana jijini Dar es Salaam baada ya kupokea Tuzo hiyo katika uzinduzi wa Tuzo za Mwajiri Bora ,Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema TCAA inafuraha kuibuka katika miongoni mwa washindi kutoka katika Upande wa taasisi za umma ambapo itakuwa chachu kwao katika kuhakikisha wanaboresha mifumo yao.

Amesema kupitia tuzo hizo watahakikisha mwakani wanafanya vizuri zaidi na kuibuka kuwa kidedea katika kuzidi kuboresha mifumo yao.”leo tulikuwa na mashindano ya kumtafuta mwajiri bora kwa mwaka 2023, jumla ya Taasisi 1000 zilishiriki katika kinyang’anyiro hiki lakini baadae 91 tu zilipitishwa kwenye hatua ya kwenda kupekuliwa na kukaguliwa zaidi kuona namna kama vile walivyojaza katika madodoso yapo sawa lakini baadae taasisi 14 tu zilienda katika hatua ya mwisho na kupatikana kwa mshindi kati ya hizo ya kwetu pia imekuaje miongoni mwao,”amesema.

Amesema kwa mwaka 2023,TCAA imefanya mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha mifumo ya kusimamia rasilimali na sera nzuri za kusimamia rasilimali watu katika kuhakikisha mikakati mbalimbali ya imewekwa katika kutekeleza sera za rasilimali za watu.

Johari amesema miongoni mwa sera za rasilimali za watu zinazotekelezwa ni pamoja na masuala ya maslahi ya wafanyakazi kuyaweka vizuri kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa na hali na morali na taratibu zote.

“Wananchi watarajie huduma bora kwa sababu tuzo hizi zitaongeza chachu yakuendelea kufanya kazi vizuri tunashukuru ate kuandaa mashindano haya,amesema