December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bima ya Mkono wa Pole ya NMB inavyoleta matumaini kwa Wanavikundi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

 Mwanakikundi anaweza kuchangia kwanzia Sh.500 mpaka Sh.2,000 kila mwezi na kupata fidia pale janga
la kifo litakapotea kwanzia Sh. 1,000,000 mpaka Sh.5,000,000.
 Bima hii imegawanyika katika makundi mawili yaani kifurushi vilivyo na wazazi na vifurushi na visivyo na
wazazi
 Kila kifurushi kina aina tatu ambavyo ni Shaba, Fedha na Dhahabu.
 Kikundi kinatakiwa kuchagua kifurushi kimoja kwa wanakikundi wote.
Benki ya NMB ikishirikiana na makampuni zaidi ya 10 ya Bima nchini, imekuja na huduma mbalimbali za bima kwa
lengo la kumlinda mteja pale majanga yanapotokea.
Moja ya bima inayotolewa ni bima ya Mkono wa Pole kwa wanakikundi kuanzia watano na kuendelea wenye umri
wa miaka 18 mpaka 75.
Bima hiyo imegawanyika katika vifurushi vya aina tatu ambavyo ni shaba, fedha na dhahabu, ambayo inamnufaisha
mwanakikundi, wenzi na watoto pale janga la kifo litakapotea.
Katika kifurushi cha Bronze (Shaba), mwanakikundi mkuu atakuwa anachangia Sh.500 kwa mwezi ambapo yeye,
mwenzi na watoto wake watapata Sh.Milioni 1.
Katika kifurushi cha Silva (Fedha), mwanakikundi atachangia Sh.1200 na iwapo akifariki atapata Sh.Milioni 3,
mwenzi Sh.Milioni 2 na watoto Sh. Milioni 1.
Aidha, kifurushi cha Gold (Dhahabu), mwanakikundi atachangia Sh.2,000 kwa mwezi na iwapo atafariki atafidiwa
Sh.Milioni 5, mwenzi Sh. Milioni 4 na watoto Sh. Milioni 1.
Kuhusu vifurushi vinavyojumuisha wazazi , kutakuwa na makundi matatu yale yale ambapo katika kifurushi cha
Shaba mwanakikundi atachangia Sh. 2,000 kwa mwezi na iwapo atafariki, Bima itatoa Sh. Milioni 1 kwake, kwa
mwenzi, watoto, wazazi na wakwe.
Katika kifurushi cha Fedha mwanakikundi atatakiwa kuchangia Sh.5000 kwa mwezi na iwapo atafariki bima itatoa
Sh. Milioni 3, mwenzi Sh. Milioni 2 na watoto, wazazi na wakwe Sh. Milioni 1.
Katika kifurushi cha Dhahabu mwanakikundi atachangia Sh.8000 na iwapo atafariki atapewa Sh.Milioni 5, mwenzi
Sh.Milioni 4, watoto Sh.Milioni 1 na wazazi na wakwe Sh.milioni 1.5.
Mahitaji ya kununua bima hii ni;

  • Kikundi kiwe na watu kuanzia watano
  • Kivuli cha kitambulisho chochote kinachotambuliwa na serikali mfano NIDA, leseni ya udereva n.k ya kila
    mwanakikundi
  • Orodha ya wanakikundi
  • Gharama ya malipo ya bima ya mwaka ( gharama italipwa kwa mwaka moja)
    Tembelea tawi la NMB karibu nawe kujipatia Bima hii au kwa taarifa zaidi wasaliana na NMB huduma kwa wateja
    0800002002.