December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Billnass: Tuthamini ndugu kuliko marafiki

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa muziki wa rap nchini, Willim Lyimo maarufu kama ‘Billnass’ amesema, Binadamu anatakiwa kuthamini sana ndugu zake kuliko marafiki, kwani ndugu ni watu ambao Mwenyezi Mungu amewachagua kuwa nao karibu.

Akiweka wazi hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Billnass amesema, licha ya marafiki kuwa watu ambao mara nyingi huwa unakuwa nao lakini hawawezi kuwa kama ukaribu wa ndugu.

“Marafiki ni watu ambao tunachagua kuwa nao. Ndugu ni watu ambao Mwenyezi Mungu amechagua tuwe nao!!. Jitahidi sana marafiki zako wafikie level ya kuwa ndugu ila usiwaache ndugu zako sababu ya marafiki!!,” amesema Billnass.