Na Esther Macha,Timesmajira,Online,Dodoma
SHILINGI Bilioni 2.4 zinatumika kukamilisha mradi mkubwa wa maji uliopo eneo la Ihumwa jijini Dodoma ambao utahudumiwa wakazi wasiopungua 15000 katika maeneo ya Nzuguni, Kisasa, Mwangaza, Stendi ya nanenane, Njedengwa na Soko la Ndugai.
Hayo yamebainishwa na Mhandisi msimamizi wa Mradi huo, James Ryoba wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ambao walitembelea mradi huo, alisema mradi huo mkubwa wa maji una uwezo kuzalisha lita 240000 kwa saa.
Mhandisi ,Ryoba amesema mradi huo ambao umekamilika kwa asilimia 95 utaanza kutumika mwanzo mwa mwezi Julai na kwamba zimebaki mita 700 kukamilika ili uanze kufanya kazi.
Mradi wa Ihumwa- Njedengwa ni miongoni mwa ,miradi mikubwa inayotekelezwa na Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Dodoma (DUWASA) ili kuwafikia na kuwahudumia wakazi wote wa Dodoma.
“Jumla ya visima saba vinapeleka maji katika mradi huu zipo changamoto ambazo zilichelewesha kukamilika mapema kwa mradi ambapo kipande cha kilomita mbili kilichelewa kutokana na mradi kupita katika makazi ya watu hivyo tulilazimika kuhamisha mabomba na kuyapeleka maeneo mengine ya wazi,” amesema Mhandisi Ryoba.
Katika hatua nyingine, Mhandisi wa usanifu na Ujenzi miundombinu ya maji taka, Aloyce Emirani amesema kwa sasa wanakabiliwa na miundombinu ya maji taka ambapo ni asilimia 20 tu ya mitambo ya maji waliyonayo.
Hata hivyo Mhandisi Ryoba amesema kuwa kulingana na idadi ya watu ilivyo sasa ilitakiwa Jiji la Dodoma liwe na mifumo isiyopungua 10 ya mitandao ya maji taka ukilingalisha na sasa kuna mitambo minne yenye urefu wa mita 200 kwa 200.
More Stories
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi