November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bilioni 15 kusaidia kutatua migogoro ya wanyama na binadamu kwenye hifadhi

Na Mwandishi wetu, timesmajira

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania ,Regine Hess, wameshuhudia kusainiwa kwa Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Bilioni 15 (Euro milioni 6) wa kusaidia Tanzania kupambana na wanyama waharibifu katika maeneo ya kusini mwa Tanzania.

Mkataba huo umetiwa saini na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi na Dkt. Mike Falke, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Ujerumani nchini (GIZ).

“Kusainiwa kwa mkataba huu ni ishawa kuwa Serikali imeanza na itaendelea kulipa uzito suala la uhufadhi na hasa kupunguza athari za wanyama waharibifu kama tembo kwa kushirikiana na wadau kama mnavyoona hapa leo,” amesema Waziri Mchengerwa.