Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
KATIKA mwaka wa fedha 2022/23 Serikali ilitenga Shilingi Bilioni 103 kwa mwaka kwa ajili ya ujenzi wa vyuo vipya 64 vya Wilaya na kimoja cha Mkoa wa Songwe, ambavyo vitachangia ongezeko la udahili wa wanafunzi 89,700.
Hayo yameelezwa jijini hapa leo,Machi 3,2025 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stad (VETA),Anthony Kasore,qakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Mamlaka hiyo kwenye kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Sulihu Hassani.
Amesema kuwa Kwa sasa, VETA ina vyuo 80, mwishoni mwa mwaka huu (2025) vyuo vinavyojengwa vinatarajiwa kukamlika na kuwezesha kuwepo kwa vyuo 145 ambavyo vitakuwa mkombozi kwa vijana wa Kitanzania na watu wazima wanaoeleka kustaafu.
Akielezea mafanikio ya Mamlaka hayo amesema kuwa Serikali kupitia VETA imefanya upanuzi wa miundombinu ya kutolea elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini kwa kutoa fedha ili kuongeza majengo mapya na ukarabati wa majengo ya zamani ili kuweka mazingira wezeshi ya kukuza ubora wa mafunzo na kuongeza fursa za udahili katika vyuo vya VETA.
Akizungumzia eneo la upanuzi na uboreshaji wa Miundombinu Mkurugenzi Mkuu amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne, Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 14.2, ambazo zimewezesha uboreshaji na upanuzi wa miundombinu ya vyuo.
Amevitaja vyuo nifaoka kuwa ni chuo cha Newala, Ngorongoro, Moshi, Dar es Salaam (Changombe), Kipawa, Mtwara, Mwanza, Mikumi, Karagwe, Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro (MVTTC) Kihonda, Nkasi, Nyamidaho, Kanadi, Ileje, Namtumbo, Mabalanga, Gorowa, Arusha na Busokelo.
Akizungumzia juu ya kuongezeka kwa Udahili na Uhuishaji wa Mitaala
amesema katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita (2021 hadi 2024), jumla ya vijana 295,175 wamedahiliwa katika vyuo vya VETA katika kozi za muda mrefu na muda mfupi.
Kuhusu urasimishaji wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo amesema kuwa kupitia Mpango wa Utambuzi na Urasimishaji Ujuzi (Recognition for Prior Learning) uliopatikana nje ya mfumo rasmi, katika kipindi cha Mwaka 2021 hadi 2025, jumla ya wanagenzi 5,175 walitambuliwa na kurasimishiwa ujuzi wao.
Amesema kati ya yao wanagenzi 1,164, walikuwa wanaoshiriki miradi ya kimkakati ya Ujenzi wa Reli ya Mwendokasi (SGR) na Bwawa la la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) na 214 waliopo kwenye vyuo vya kurekebisha tabia (wafungwa katika Magereza) vya Ukonga, Arusha na Morogoro.
Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

More Stories
Bilioni 3 kukamilisha ujenzi shule amali Kata ya Choma
Serikali yatoa fursa kwa wahitimu kidato Cha nne 2024 kubadilisha Tahasusi
Masache asema CCM Mbeya kimepoteza mtu muhimu