December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Betika yazindua SODO 4 C LIMATE

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kampuni ya michezo ya kubashiri Tanzania Betika kampeni ya Sodo 4 Climate, katika kampeni hii betika wanahamasisha utunzaji wa mazingira kupitia mchezo wa sodo.

Kauli mbiu ya kampeni hii ni “Shabikia soka sio uharibifu wa mazingira”.

Meneja mkuu wa betika Bw.Tumaini Maligana katika uzinduzi huo alisema kwamba “ Lengo ni kupambana kupunguza mabadiliko ya tabia za nchi kwa ujumla, kupitia utunzaji wa mazingira basi tutahakikisha hali ya hewa nzuri, afya bora na pia maendeleo katika jamii yetu”.

Katika sodo 4 climate itachezeka ligi katika soka la ufukweni pale uwanja wa coco beach ambapo Betika wamealika jumla ya timu 8 zitakazoshiriki na ligi hii itaenda kwa muda wa takribani wiki saba. Ligi hii itahusisha team zifuatazo, Betika staff fc, Coco beach FC, RC FC , Tulia trust foundation FC, Espanyol fc, Bodaboda msasani fc, Ipp media.

Katika ligi hii pia kila team watakua na team za wanawake na wanaume ambazo kila jumamosi kutakua na mechi moja ya wanawake na mechi moja ya wanaume.


Ufunguzi wa ligi hio ulitanguliwa na usafishaji wa mazingira kwa ujumla na pia kutoa elimu kuhusiana na swala zima la kuhifadhi taka katika maeneo husika. Katika kipindi cha wiki zote saba za ligi hii kutakua na matukio mbali mbali ya utunzaji wa mazingira na maendeleo ya kijamii kwa ujumla.

Bwana Tumaini Maligana pia allimalizia kwa kuwatakia kila la kheri timu zote zitakazo shiriki katika ligi hii ya Sodo 4 Climate kwa sababu betika watatoa zawadi za kutosha kwa wale watakaofika fainali ya Sodo 4 Climate.

Mechi ya ufunguzi ilikua Betika staff fc 1- 3 Coco Beach FC.