January 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

‘Twenzetu Ivory- Coast ki-VIP’ yazinduliwa

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

IKIWA imebakia mwenzi mmoja kuanza Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yanayotarajiwa kuanza January 13,2024 Jijini Abdjan Ivory Coast Kampuni ya Kubashiri Tanzania Betika kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tigo imezindua Kampeni kubwa ya “Twenzetu Ivory -Coast Ki-VIP”.

Akizungumza leo Desemba 6, 2023 Jijini Dar es salaam Afisa Habari Betika Tanzania Rugambwa Juvenalius amesema Kampeni hiyo ni kwa ajili ya wateja wa Betika wanaotumia Mtandao wa Tigo hivyo wanaendelea kuwajali kwa kuwapa huduma bora ambapo promotion hiyo nzuri itaambatana na zawadi za kutosha kwa watanzania kuanzia msimu huu wa sikukuu mpaka Michuano yenyewe.

“Tembelea tovuti ya Betika www.betika .co.tzvilevile unaweza kuingia kwenye drop kwa kubeti kupitia huduma y SMS tuma neno BETIKA kwenda 15316 sambamba na hilo unaweza kubeti kwenye menyu ya kupiga 14916# weka pesa kwenye akaunti yako ya Betika kwa kutumia Tigo pesa na ufanye ubashiri kila siku ili uweze kujishindia zawadi kibao na kupata fursa ya kushuhudia Michuano mikubwa wa soka barano Afrika”amesema Rugambwa

Hata hivyo amesema Mabongwa watapatikna kwa njia ya droo za kila siku na droo kubwa ya wiki itakuwa kila jumatatu wadau wanachotakiwa ni kubashiri mechi mbalimbali kila siku na mabingwa wa droo ya wiki watatangazwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram na Facebook

Rugambwa amesema Droo kubwa ya kupata Mabingwa 6 watakaoenda Ivory Coast itanyika January 1, 2024 na Mabingwa hao watapata huduma za Ki-VIP kuanzia wakiwa Tanzania mpaka kufika Ivory Coast ambapo watapatiwa tiketi za ndegw kwenda na kurudi ,hoteli kwa siku zote Ivory Coast na usafiri wa kifahari kuelekea uwanjani na tiketi za kutazama mechi Uwanjani, hivyo wateja wote mnakaribishwa kutumia fursa hiyo.

Naye Meneja Biashara Tigo Pesa Fabian Felician amebainisha kuwa promotion hiyo itakuwa pia na zawadi ikiwemo TV Hisense yenye nchi 70 kila wiki kwa washindi wawili zikiambatana na Ving’amuzi vya DStv na kifurushi cha mwezi mmoja hivyo mamilioni kushindaniwa kwenye droo za kila siku na zawadi kubwa nono.

Meneja biashara wa Kampuni ya simu Tigo Fabian Felician akizungumza machache mara baada ya kuzinduliwa kwa Kampeni ya “Twenzetu Ivory Coast Ki-VIP ” kushuhudia michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika
Afisa Habari Rugambwa Juvenalius akizungumza na Wanahabari Leo Disemba 06,2023 Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzindua Kampeni ya “Twenzetu Ivory-Coast Ki-VIP ” kwa kushirikiana na Kampuni ya simu Tigo kupitia tigopesa.
Balozi wa Kampuni ya kubashiri nchini Betika Mchekeshaji maarufu kama “Kiredio” akiongea machache huku akihaidi atafikisha zawadi za TV na King’amuzi kwa washindi wa kampeni hiyo