Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) imezindua wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam ikiwa na lengo la kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake .
Katika wiki hiyo Benki itajikita kutoa huduma kwa wafanyabiashara wadogo na wakati (SME’s)
Akizungumza katika uzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Lilian Mtali alisema kuwa Benki hiyo imefanya uboreshaji mbalimbali katika utoaji huduma zake ikiwemo matumizi ya mifumo yote ya malipo ya Serikali.
“Sasa hivi tunakamikisha mfumo wa Tausi kwahiyo wanaofanya kazi na Halmashauri hakutakuwa tena na changamoto za malipo kwa sababu mifumo yote tunayo” alisema Mtali.
Alisema kuwa katika miaka 99 ya utoaji huduma tangu kuanzishwa kwake TCB imekuwa ikishirikiana na taasisi mbalimbali binafsi na za serikali ikiwemo Kampuni za Bima kwa ajili ya usalama wa mteja na biashara zao.
“Mfano ukipata changamoto katika biashara yako au wewe mwenyewe binafsi tunajua kwamba washirika wetu watasaidia kuhakikisha biashara na familia yako inaendelea” alisema.
Mtali alisema kuwa TCB itatumia wiki hiyo ya huduma kwa wateja kukusanya maoni na kufanya majumuisho kuhusu huduma zitewazo na benki hiyo.
Alisema kuwa malengo ya benki hiyo ni kuwa juu ya benki tatu kubwa nchini katika kipindi cha miaka michache ijayo.
Aidha ameishuru Serikali kwa kuiunga mkono Benki hiyo kwa kipindi chote tangu kuanzishwa kwake na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii.
“Tumekuwa na safari ndefu tumeweza kufikisha miaka 99 tunashukuru Mungu kwa hilo wateja wetu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweza kutusaidia Benki yetu mwanzo hadi kufika sasahivi” alisema.
Akizungumza katika uzinduzi huo mmoja wa wateja wa benki hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ubx Tanzania, Seronga Wangwe aliishukuru TCB kwa kuendelea kuwaamini wafanyabiashara kwa kuwapatia mikopo ambayo inasaidia kuimarisha biashara zao.
“Kuna benki zingine zilikuwa zinatukataa lakini TCB walitukibali na wametufanya tuendelee kama Kampuni hadi leo naimani na wengine wamepitia hali ya kuaminiwa kama sisi” alisema Wangwe.
More Stories
The Desk & Chair yashusha neema Gereza la Butimba
TVLA,yapongezwa kwa kuzalisha chanjo
TAKUKURU,yasaidia kurejesha hekali 8