Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga
Mjasiriamali Ally Athuman Mnyone mkazi wa Same ameibuka na ushindi wa pikipiki ya miguu mitatu maalumu kwajili ya kubebea mizigo kwenye Kampeni ya bonge la mpango inayoendeshwa na benki ya NMB.
Akizungumza mara baaya ya kupata zawadi hiyo mshindi huyo ameonyesha kufurahishwa na zawadi hiyo na kusema kuwa pikipiki hiyo itamsaidia kumuinua kiichumi.
Mjasiriamali huyo amewataka wateja wenzake kuendelea kuweka pesa zao katika benki hiyo huku akiwaaminisha kuwa jambo hilo linafanywa kwa uadilifu na kwamba hakuna udanganyifu wa aina yeyote ile.
“Nataka niwaaminishe watu kwamba hii kampeni ya bonge la mpango haimpendelei mtu yeyote na wala haina udanganyifu wowote mimi watu hawa hawanijui wala mimi siwajui lakini leo hii nimeibuka na ushimdi huu ambao kwangi mimi naona ni hatua kubwa nimeipiga kimaisha, “alisisitiza Mjasiriamali huyo.
Dismas Prosper ni Meneja wa Nmb kanda ya kaskazini amesema kampeni hiyo inatokana na faida waliyoitengeneza kama benki kurudisha sehemu ya faida kwa wateja wao.
Meneja huyo amesema kuwa benki hiyo ilitenga zaidi ya shilingi milioni 300 kama zawadi zikiwemo pikipiki za miguu mitatu za mizigo aina ya Skymark pikipiki 50 ambapo kampeni hiyo inamuwezesha mtanzania yeyote aliyekuwa na akaunti ya NMB au alifungua akaunti mpya na akajiwekea angalau shilingi laki moja wameweza kujiweka kwenye utaratibu wa kupata zawadi.
“Kampeni ya, bonge la mpango awamu ya pili ambayo imelenga sana kuhamasisha wananchi na watanzania kwa ujumla kuweka akiba kwenye mazingira salama hasa benki ya NMB, “amebainisha Meneja huyo.
Ameongeza kuwa kila wiki kaika kipindi cha miezi mitatu tulichokuwa tunacheza jii kampeni ya bonge la mpango toka mwezi wa kumi wateja 10 walikuwa wanajishindia fedha taslimu na wateja wawili walikuwa wanajipatia pikipiki hizi za mizigo za miguu mitatu aina ya skymark lakini kila mwisho wa mwezi kampeni hii iliyokuwa ikichezwa wateja watatu walikuwa wanaondoka na pikipiki za aina hii, “amesisitiza Dismas.
Aidha meneja huyo wa kanda amewahamasisha watanzania kuendelea kujiwekea akiba kwenye akanti zao ndani ya benki hiyo ili waweze kupata nafasi kushinda zawadi mbalimbali kutoka katika benki hiyo.
Jumla ya zawadi zenye thamani ya shilingi milioni 300 zimeolewa na benki ya NMB kwajili ya wateja wao ambapo zawadi hizo ni pamoja na pikipiki za miguu mitatu kwajili ya kubebea mizigo.
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi