January 7, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Benki ya NMB yakabidhi jezi, madawati Zanzibar

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Katika kusherehekea maadhimisho ya safari ya mafanikio ya miaka 25 ya NMB visiwani Zanzibar, benki hiyo imeigusa jamii kwa kukabidhi jezi kwa ajili ya vikosi vya michezo Sita, vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, lakini pia madawati 407 kwa ajili ya Taasisi ya Karume Sayansi na Teknolojia (KIST), Shule za msingi Makandara, Kidimni, Uzini pamoja na Maandalizi.

Msaada huu umepokelewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar – Mhe. Hemed Suleiman Abdullah, akiwa amekabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB – Ruth Zaipuna aliyeambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya NMB – Dkt. Edwin Mhede.

Akizingumza wakati wa makabidhiano, Bi.Ruth aliiahidi Serikali ya Zanzibar ushirikiano endelevu katika kuharakisha ukuaji wa Uchumi wa Buluu, huku akifichua kuwa mwaka huu, NMB imetenga Sh. Bilioni 6.2 kurejesha kwa jamii, zikiwamo Sh. Bilioni 2 za Kampeni ya Kitaifa ya Upandaji miti, sanjari na elimu ya mazingira kwa wanafunzi wa Shule za Msingi 189 Bara na Visiwani Zanzibar, zinazoshiriki Shindano la ‘Kuza Mti Tukutuze’
 
Aliongeza kuwa, kiasi hicho cha Sh. Bilioni 6.2 ni Zaidi ya mara tatu ya ilichotumia mwaka 2021 cha Sh. Bilioni 2 za Programu ya Uwajibikaji kwa Jamii, huku mwaka 2022 ikitumia kiasi cha Sh. Bilioni 2.9, lakini mafanikio ya faida baada ya kodi ya Sh. Bilioni 429, yakawezesha kuongeza kwa fungu la kurejesha kwa jamii.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar – Mhe. Hemed Suleiman Abdullah, baadhi ya madawati kati 407 yaliyotolewa na NMB kwa Taasisi ya Karume Sayansi na Teknolojia (KIST), Shule za msingi Makandara, Kidimni, Uzini pamoja na Maandalizi. Wakishuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya NMB – Dkt. Edwin Mhede (pili kushoto), Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar – Mhe. Zubeir Ali Maulid (Kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi – Idrisa Mustafa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar – Mhe. Hemed Suleiman Abdullah, baadhi ya jezi kwa ajili ya vikosi vya michezo Sita, vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Wakishuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya NMB – Dkt. Edwin Mhede (pili kushoto), Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar – Mhe. Zubeir Ali Maulid (Kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi – Idrisa Mustafa.