Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Benki ya NMB imekuja na bima ya mali ambayo ni maalum kwa ajili ya kulinda mali zako dhidi ya majanga yatakayotokea ikiwa ni pamoja na jengo na vitu vya ndani ikiwemo samani.
Bima hii inamkinga mteja dhidi ya majanga yatokanayo na moto,radi, tetemeko la ardhi, mlipuko wa Volkano , mafuriko, maandamano na migomo yasiyo ya kisiasa, kupasuka au kufurika kwa tanki la maji, bomba au vifaa vyake.
Aidha, wizi wa kutumia nguvu za kuingia kwenye jengo na kuiba, madhara kwa majengo kutokana na chombo cha moto au wanyama wasiomilikiwa na mwenye bima.
Kwa upande wa viwango vya bima, vinatolewa kulingana na thamani iliyowekwa katika bima, inategemea na gharama elekezi inayotolewa na mamlaka ya usimamizi wa bima (TIRA).
Mfano;
Thamani ya nyumba(Tshs) | Tshs. 100,000,000 |
Agizo la kiwango(%) cha chini 2018 ni 0.15 | 0.15 |
Kiwango bila VAT | Tshs. 150,000 |
Pamoja na VAT 18%(Tshs) | Tshs. 27,000 |
Kiwango(Pamoja na VAT) | Tshs. 177,000 |
Unachohitaji;
- Umiliki na Kitambulisho halali
- Fomu ya gharama na viwango
- Orodha ya vitu na gharama zake
- Thamani ya mali
Janga litakapotokea, toa taarifa za madai katika tawi lolote la NMB karibu yako piga simu namba 0800 002 002 bure!
Pia, ambatana na ripoti ya polisi katika masuala ya wizi(loss report) au ripoti ya jeshi la kuzima moto na gharama za marejesho/marekebisho.
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi