Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Benki ya NMB imeingia makubaliano na Mamlaka ya Hifadhi Mji Mkongwe, chini ya usimamizi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuboresha bustani ya Forodhani.
Chini ya makubaliano hayo, Benki ya NMB itasimamia vipengele vifuatavyo:
✅ Kuhakikisha uwepo wa huduma na suluhishi za kifedha, elimu za kifedha na mikopo kwa wafanyabiashara wa Forodhani.
✅ Kuweka maeneo maalum ya polisi, kubadilishia nguo wapiga mbizi na NMB Wakala.
✅ Kuboresha maeneo ya kupiga mbizi Forodhani, na kutoa maboya kwa wapigambizi kwa ajili ya usalama wao.
✅ Kuboresha taa zilizopo eneo la Forodhani.
Makubaliano haya yametiwa saini na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi Mji Mkongwe, Eng. Ali Said na Afisa Mkuu wetu wa Wateja Binafsi na Biashara – Filbert Mponzi huku wakishuhudiwa na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mhe. Simai Mohamed Said na viongozi wengine.
More Stories
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi
Kampeni ya Sako kwa Bako yawafikia Kanda ya Kati