January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Benki ya NMB yafadhili mkutano wa wahariri Mogogoro

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia, Nape Nnauye (katikati) akiteta Jambo na Kaimu Meneja tawi la NMB Wami Paul Nyoni baada ya kupokea Cheti cha shukrani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 12 wa mwaaka wa kitaaluma wa wahariri wenye kauli mbiu ya “Sheria ya habari na maendeleo ya vyombo vya habari” unaofanyika mkoani Morogoro. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deudatus Balile na Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Bakari Machumu (kulia kabisa). Benki ya NMB ilishiriki kama mdhamini kwenye mkutano huo unaoendelea hoteli ya Morena, Morogoro
Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari, Nape Nnauye akimkabithi Kaimu Meneja tawi la NMB Wami Paul Nyoni (kulia) Cheti cha shukrani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 12 wa mwaka wa kitaaluma wa wahariri wenye kauli mbiu ya “Sheria ya habari na maendeleo ya vyombo vya habari” unaofanyika mkoani Morogoro. Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deudatus Balile (kushoto) na Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Bakari Machumu (wapili kulia). Benki ya NMB ilishiriki kama mdhamini kwenye mkutano huo unaoendelea hoteli ya Morena, Morogoro.