January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Benki ya NBC yaandaa chakula cha jioni kwa wateja wake, wajadili matarajio ya siku zijazo

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

BENKI ya NBC yaandaa Chakula cha Jioni kwaajili ya wateja wake katika hoteli ya Hyatt Regancy the Kilimanjaro jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kwajili ya kujadili matarajio ya siku zijazo.

Katika Chakula hicho cha jioni kuliundwa jukwaa la benki hiyo kwaaajili ya Kubadilishana mawazo na kujadiliana na wateja wake changamoto zinazowakabili.

Hata hivyo waliangalia malengo yajayo benki hiyo baada ya kudorora kwa biashara kwa miaka miwili kutokana na janga la Covid-19.

Mkurugenzi Mkuu wa NBC Tanzania, Theobald Sabi akiongozana na Mtendaji Mkuu wa Uendeshaji wa ABSA Kanda iliwakaribisha watendaji wakuu wa biashara kutoka viwanda 50 nchini kwa lengo la kufungua fursa za biashara katika soko la Afrika.