Na Yusuph Mussa, TimesMajira Online, Arusha
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imeahidi kuendelea kuunga mkono Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM) kwa ajili ya uwezeshaji na kuongeza huduma zake kwa kufungua matawi kwenye ngazi ya wilaya na halmashauri ili kuifikia jamii kwa karibu.
Hayo yalisemwa Mei 29, 2023 na Mkurugenzi wa Benki ya NBC anaeshughulikia wateja wa rejareja Elibariki Masuke kwenye Mkutano Mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika jijini Arusha, ambapo Benki ya NBC ni miongoni mwa wafadhili wakuu wa mkutano huo.
“Tunakiri kazi nzuri iliyofanywa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (MSM) katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu. Kazi bora imefikia na kunufaisha idadi kubwa ya Watanzania. Kama benki kongwe nchini tunaahidi kuendelea kusaidia na kutoa suluhisho za kibenki zinazohusiana na mahitaji kwa jamii yetu” alisema Masuke.
Masuke alisema, Benki ya NBC pia ni moja ya walipa kodi wakubwa nchini, na wamelipa zaidi ya sh. bilioni 66.5 serikalini kwa mwaka 2022. Katika kipindi hicho hicho, benki ililipa gawio la Serikali lenye thamani ya bilioni sita.
“Tunajivunia kuwa mshirika muhimu na mshiriki katika ajenda ya maendeleo ya kitaifa, na tunaahidi kuendelea kuunga mkono. Milango yetu inabaki wazi kutumikia sio tu Serikali na watumishi wa umma, lakini Watanzania wote kwa ujumla” alisema Masuke.
Alisema Benki ya NBC inatoa suluhisho anuwai za ubunifu za suluhisho za kielektroniki kwa Halmashauri za Wilaya na Manispaa katika ukusanyaji wa mapato na suluhisho za malipo ambazo zitarahisisha huduma za kibenki.
“Malipo ya kielektroniki ya Benki ya NBC na suluhisho za kukusanya mapato zinawapa MSM malipo salama na uwezo wa usimamizi wa makusanyo ambao hufanya malipo kuwa rahisi. Hivi karibuni benki imeanzisha suluhisho la malipo kwa kutumia mtandao ulioitwa “The NBC Connect’ kwa malipo rahisi mtandaoni. Benki hiyo pia hutoa suluhisho nyingi za mikopo ili iweze kutimiza mahitaji ya mashirika kampuni, na watu mmoja mmoja.” alisema Masuke.
Masuke alisema pia Benki ya NBC inafadhili kwa dhati miradi ya kimkakati ikiwemo reli ya SGR. Wamekuwa pia wakisaidia vikundi maalumu na kuongeza mnyororo wa thamani kwenye Kilimo, AMCOS, Wamachinga, bodaboda, na wafanyabiashara ndogondogo.
Masuke amesema kuwa matawi yote ya Benki ya NBC yana vifaa vya kutosha kutimiza mahitaji ya kifedha ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Masuke alisema Benki ya NBC ni miongoni mwa benki za kibiashara nchini wakiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 50 katika kutoa huduma za kifedha. Pia inajivunia mtandao wa matawi uliopanuliwa wa matawi 49 na ATM zaidi ya 200 zilizowezeshwa na Visa. Benki hiyo pia ina vituo vya kutoa huduma za kifedha zaidi ya 800, na zaidi ya mawakala 9,000 kote nchini. Benki pia imeajiri zaidi ya wafanyakazi 1,200.
Masuke alisema pia Benki ya NBC ni Mfadhili Mkuu kwenye Lgi Kuu nchini maarufu kama NBC Premier League, ambayo hutoa ajira na kuchochea shughuli za kiuchumi.
More Stories
Wanafunzi 3000 wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Mkutano Mkuu maalumu CCM wapitisha Rais Samia ‘mitano tena’ Balozi Nchimbi aula
Dkt.Kikwete:Ushindi wa CCM ni lazima