Na Jackline Martin, TimesMajira Online
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar SMZ imesema kwamba itaendelea kutumia Mchezo wa Mpira wa Miguu katika kutangaza Utalii pamoja na kutangaza Sera ya Uchumi wa Buluu.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Simai Mohammed Said Wakati akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi katika Ufunguzi wa Kongamano la Pili la Mipira wa Miguu Tanzania lililofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Goldern Tulip Uwanja wa Ndege Mjini Unguja.
Waziri Simai aliesema kupitia Kongamano hilo la Mpira wa Miguu Tanzania, Serikali zote mbili wameamua kutangaza Utalii pamoja na Sera ya Nchi ya Uchumi wa Buluu.
“Kwa niaba ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar lakini pia kwa niaba ya serikali zote mbili sisi tumefurahi leo kuona kwamba mkutano huu wa Tanzaia football summit wa pili umefanyika na umeleta viongozi mashuhuli, makocha na watu mashuhuri katika mchezo”
Nae Rais wa Shirikisho la Soka Visiwani Zanzibar Abdullatif Ali alisema kwamba Kongamano hilo litatoa fursa kwa vijana wenye vipaji kwenda Nnje kucheza Soka pamoja na kuimarisha Timu za Taifa za Tanzania.
“Vijana wadogo wenye vipaji vya mpira wa mguu, wageni wetu hawa wamekuja kwaajili ya kwenda kuona ujuzi huo na pengine kuchukuliwa kwenda nje ya nchi kuendeleza vipaji vyao na kuimarisha timu za Taifa za Tanzania”
Mwakilishi kutoka Benki ya KCB Kitwana Mitto alisema wao kama KCB wamekuwa wakishiriki kwa ukubwa zaidi kama wadau na wadhamini katika mchezo wa mpira wa miguu lakini siyo katika mpira wa miguu pekee bali hata katika kutangaza sera ya uchumi wa Buluu.
Kwa Upande Wake Mshiriki wa Kongamano ambae ni Mkurugenzi wa Hlamshauri ya Mji wa Geita na Mmiliki wa Timu ya Geita Gold Zahra Michuzi alieleza umuhimu wa Kongamano hilo
katika kukuza Mpira wa Miguu Nchini;
“Kongamano hili limetoa hamasa, limeonesha tija na namna bora ya uwekezaji katika soka, limetupa mwanga la namna bora ya kufanya mikataba yetu ili kuepukana na kulipa fidia sehemu ambayo hatukutakiwa kufanya hivyo”
Aidha alisema anaamini kupitia Kongamano hilo litatoa ari kuhakikisha kwamba wanatengeneza wachezaji watakaofikia viwango vya masoka ya kimataifa.
Kongamano hilo la Siku mbili ambalo limewashirikisha wadau wa Soka kutoka Nchi zaidi ya 14 Afrika Duniani ambalo limefadhiliwa na Benki ya KCB pamoja na Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Zanzibar.
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi