Na Penina Malundo,Timesmajira
WAWEKEZAJI kutoka nchi 15 kutoka nchini ya Tanzania,Ulaya,Nchi ya Uarabuni pamoja na Marekani wamekutana nchini kwa lengo la kukutana pamoja na kujadili namna wanaweza kukuza biashara zao ikiwemo uwekezaji nchini Tanzania pamoja na kupanua masoko ya wafanyabiashara hao ndani na nje ya nchi zao.
Hatua hiyo imekuja baada ya Benki ya Equity kuwakutanisha wawekezaji hao kwa lengo la kuongeza thamani za biashara ili kufanya uchumi wa nchi zao kuimarika na kuvutia wawekezaji.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),Prof.Tandi Lwoga ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara,Dkt. Selemani Jafo, aliipongeza benki ya Equity kuwa kiunganishi wa wawekezaji hao na wafanyabiashara kusaidia kuwakutanisha kwa pamoja na kuona upatikanaji wa masoko na mikopo ili kuwasaidia katika bidhaa mbalimbali wanazoziwekeza.

Amesema Equit imefanya kazi kubwa ambayo ilianza kufanywa tangu mwaka 2022 na imekuwa ni Jukwaa nzuri la kuwakutanisha wafanyabiashara wa ndani na nje.”Hii ni fursa ya kuongeza uwekezaji nchini ambapo wanaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuvutia uwekezaji na kuwekeza Tanzania.
”Ni fursa kubwa ambayo Tanzania imeipata kupitia Equity Bank kwaajiliya kuweza kuwaleta wawekezaji na kuja kuwekeza katika sekta tofauti tofauti ikiwemo ya Kilimo,Utalii,Usafirishaji ,Ujenzi na Seta nyingine zote zitakazoenda kuchangia kuinua uchumi nchi,”amesema.

Amepongeza juhudi za benki ya Equity kwa kuwaleta wafanyabiashara na wawekezaji pamoja na kuwataka taasisi nyingine nchini za umma na binafsi kuwa kiunganishi kwa wafanyabiashara mbalimbali ili kuvutia wawekezaji zaidi kwani Tanznaia inafursa nyingi kuanzia Utalii,Kilimo,Huduma,Mawasiliano na Teknolojia.

Kwa Upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity Tanzania, Isabella Maganga amesema Jukwaa lao linalofahamika kwa jina la Trade mision ni maonesho ya kibiashara ambayo yanawakutanisha wafanyabiashara wa sekta mbalimbali kulingana na mahitaji ya soko,mazingira ya kiuchumi na fursa zilizopo.
Amesema wafanyabiashara waliowakutanisha katika jukwaa hilo ni takribani 53 kutoka katika nchi 15 za Afrika na wengine nchi ya Ulaya,Marekani na Nchi za Uarabuni na USA huku wafanyabiashara wa kitanzania wapo wafanyabiashara 183.

”Lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara hao ni kukuza fursa za wafanyabiashara wa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania ili kuyakuza masoko yao na kuongeza thamani biashara zao na kuchukua bidhaa kupeleka nje ,tunataka kukuza biashara za nje na kufanya uchumi unakuwa na kuvutiwa wawekezaji,”amesema.

Oscar Kisanga Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Chemba ya Biashara ,Viwanda na Kilimo(TCCIA),amesema chemba yao imewapeleka wafanyabiashara waliopo katika Chama chao ambao wapo katika sekta ya viwanda,bianshara na Afya ili waweze kukutana na wenzao kutoka nchi mbalimbali ikiwemo ya Kenya na Uganda ili kufanya mashirikiano ya biashara wanazofanya,kubadilishana fursa na kutafuta masoko.
More Stories
RC Senyamule:Jamii Cup siyo burudani tu,ni chombo cha malezi
Wakulima Tabora wasifu ubora mbolea za TFC
Kongamano la kimataifa la kusoma Qur’an kufanyika Mei 24,2025