Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Katika kuunga mkono juhudi za serikali, Benki ya Equity Tanzania imesaini mkataba wa makubaliano na kampuni ya Bakhresa Group ili kuhakikisha watanzania wanapata bidhaa bora za ngano na kupambana na tatizo la lishe bora.
Akizungumza na waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam, Meneja was Biashara wa Benki ya Equity Tanzania, Leah Ayoub alisema lengo ni kuhakikisha wasambazaji wa bidhaa wanakuwa na bidhaa za kutosheleza mahitaji ya wateja na watanzania kwa gharama nafuu.
Alisema makubaliano hayo yanayowalenga wasambazaji bidhaa yamejikita katika kuboresha na kurahisisha upatikanaji wa bidhaa za Bakhresa Group na utoaji mikopo ya bila riba na kutokuwa na haja kubwa ya nyaraka kwa bidhaa hizo dhamira yao ni kutoa mikopo ya kidigitali.
“Huduma hii ya mikopo ilianzishwa haswa kuwasaidia wajasiriamali waweze kupata huduma kwa urahisi na hawana haja ya kuja benki kupata huduma na huduma hii inawawezesha hasa wasambazaji ambao wanapata huduma hasa za viwandani, nishati za gesi na mafuta”
Aidha alisema kupitia huduma hiyo msambazaji anaweza kupata huduma katika Benki ya Equity na akapewa mkopo kwa njia ya simu ya mkononi wenye makubaliano kwa muda wa siku 7-30 kutokana na elimu alipo.
Pia alisema makubaliano hayo yamejikita katika kupunguza gharama za usafiri kwa kuwapatia wasambazaji bidhaa za kutosheleza soko na maghala ya kuhifadhia lakini pia uimarisjaji wa tabia za kibenki kwa wasambazaji.
Aliongeza kuwa makubaliano hayo yamejikita katkka kuboresha na kurahisisha mifumo ya mauzo na makusanyo ya pesa katika biashara zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano kutoka Bakhresa Group aliishukuru Benki ya Equity kwa kuja na bidhaa ambayo inaenda kutatua changamoto waliyokuwa wakikutana nao wateja wao
“Jambo hili lina manufaa makubwa kwetu sisi kama wazalishaji, wafanyabiashara na wateja kwa ujumla Kwanza linapunguza gharama , inafanyika kwa haraka zaidi “
Aliwataka wateja wote ambao hawajajiunga na huduma hizo zinazopunguza gharama za uendeshaji kazi wajiunge mara moja ili kuwa na urahisi katika ufanyaji kazi zao.
More Stories
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi