Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Karume Hajji Bechina, amekabidhi Televisheni nchi 46 kwa Mashina mawili ya wakereketwa ASHANTI Sokoni na Jabari la Kiusa Ili waweze kuangalia Taarifa ya Habari na kufatilia michezo .
Akizungumza Mbele ya mgeni Rasmi mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Side ,Mwenyekiti Bechina alisema vijiwe hivyo amevikabidhi Televisheni wawe wanafatulia michezo mbali mbali ya hapa nyumbani na nje ikiwemo kufatilia Taarifa ya Habari .
“Leo nimeitisha mkutano wa Wana chi katika mtaa wa Karume mkutano wa kawaida wenye ajenda ya ikiwemo Ulinzi na Usalama ,Usafi na Mazingira ,Pamoja na kero za wananchi natumia fursa hii pia kutoa Televisheni Mbili katika vijiwe hivi vya michezo Pamoja na kugawa Zakatul Fitir wananchi wasio jiweza wakiwemo Walemavu ,Wajane ,na Wazee “alisema Bechina .
Katika kikao hicho cha Wananchi Ilala kero kubwa ambazo zimewashirishwa ni uchakavu wa Soko la Ilala Boma ,Miundombinu yake sio rafiki chakavu kupelekea maji kutuwama kama wanavua samaki ,pamoja na takataka kushindwa kubebwa kwa wakati.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde, alipokea kero za uchakavu wa Soko la Ilala Boma alisema ,Serikali ya awamu ya sita imejipanga ipo katika Mikakati ya kujenga soko hilo la kisasa kama Kisutu ,hivyo amewataka Wakazi wa Ilala kuvuta subira Serikali yetu ni Sikivu .
Aidha Mwenyekiti Said Sidde amesema mara baada kumalizika sikukuu ya Idd Fitir atakwenda kuonana na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji na Mhandisi wa Halmashauri hiyo kwa ajili ya kutatua kero za kuzibua mfumo wa mifereji ya maji wakati wakisubiri mchakato wa kujenga soko ukiendelea .
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi