Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mhe. Augustino Ramadhani amefariki Dunia leo saa mbili Asubuhi katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mtoto wa kiume wa Jaji Mstaafu wa Tanzania Augustino Ramadhani, Yakud Ramadhani ameeleza kifo cha Baba yake huyo na kusema kuwa alikuwa anasumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu, ambapo pia hata kabla ya mauti kumfika aliwahi kwenda kutibiwa nchini Kenya.
“Ni kweli amefariki leo mida ya saa 2 asubuhi, alikuwa Aga khan na baadaye akaenda Kenya kwa matibabu zaidi na baadaye akarudi nyumbani lakini akawa bado anaumwa, sasa hivi wana familia wanafanya taratibu kwa chochote kitakachotokea tutawajuza” amesema Yakud.
Aidha kwa upande wa taarifa zilizotolewa na Mahakama ya Tanzania zimeeleza kuwa Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani, amefariki Dunia leo saa mbili asubuhi katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.
More Stories
Serikali yaja na mwarobaini wa changamoto ya Kivuko Magogoni – Kigamboni
Kisarawe kukata keki ya Birthday ya Rais Samia
Wataalam wa afya wakutana kujadili ugonjwa wa Marburg