Na Mwandishi Wetu, TimesMajira, Online, Dar
AKIYEKUWA Waziri wa Fedha katika Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya uongozi wa Hayati Benjamin Mkapa,, Basil Mramba amefariki dunia jijini Dar es Salaam.
Kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, kimetokea leo kwa ugonjwa wa corona.
Taarifa iliyotolewa na mwanaye, Godfrey Mramba imeeleza kuwa baba yake amekutwa na umauti leo asubuhi wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Regency. Mramba alizaliwa Mei 15, 1940.
“Mzee amefariki mapema leo (Agosti 17), ameugua pale Regency Medical Centre muda wa wiki mbili, amepata maradhi ya Covid 19 tumempoteza leo, tunamshukuru Mungu kwa maisha yake na tutayasherehekea,” alinukuliwa akisema Godfrey wakati akizungumza na moja ya mtandao wa kijamii.
Godfrey amesema kutokana na janga la Corona msiba huo utahusisha watu wa familia pekee ili kuepuka mkusanyiko.
“Kutokana na janga hili familia inapokea salamu za pole, faraja na sala zenu ila tutaomba shughuli za msiba uwahusishe wanafamilia pekee na tutakuwa nyumbani kwa marehemu barabara ya Mawenzi Oysterbay,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Godfrey.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Rais Samia afanya uteuzi