Na Esther Macha,Timesmajira Online
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Innocent Bashungwa amesema wizara yake imetoa zaidi ya bil.243.9 kwa ajili ya miradi ya afya 233 ambapo kati ya hiyo 110 imetekeleZwa kwa awamu ya kwanza wakati mingine iliyobakia ni kwa halmashauri ambazo hazifanya vizuri nchini .
Bashungwa amesema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua miundo mbinu ya majengo katika hospitali ya wilaya Igawilo ambapo hajaridhishwa na baadhi ya miradi kutokamilika kwa wakati na kutoa muda wa` wiki moja iwe imekamilika .
“Wakuu wawilaya na wakurugenzi wa halmashauri zote nchini ambao watashindwa kutekeleza miradi ya ujenzi wa zahanati,vituo vya afya na hospitali za
wilaya ifikapo April 30 mwaka huu watawajibishgwa na kutoa sababu kwanini wasichukuliwe hatua”amesema Bashungwa.
Aidhaameagiza
wakuu wa mikoa wote nchini kuwasimwa Spika wa Bunge na Mbunge wa jimbo laMbeya Dkt. Tulia Ackson kwa kujiletea maendeleao na badala yake viongozi hao wakiwa miongoni mwa watakaochukuliwa hatua na wizara amia wakurugenzi na
wakuu wa wilaya kuhakikisha muda uliopangwa na wizara miradi yote inatekelezeka katika fedha za awamu ya kwanza ya pili .
“Nitasikitishwa na viongozi wa mkoa wa mbeya ambao watashindwa kusimamia miradi ya maendeleo kushindwa kutumia fursa za uwepo itawachukulia hatua Wakuu wa Wilaya ,Wakurugenzi wa halmashauri watakaoshindwa kukamilisha miradi ya afya ifikapo April 30 mwaka huu na kuagiza wakuu wa Mikoa nchini kuwasimamia”Amesema Waziri Bashungwa..
Hata hivyo Waziri Bashungwa amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Triphonia Kisiga kuhakikisha miradi hiyo inakwenda kwa kasi ili Mbeya ipige hatua kwani kwa sasa kama Wizara watahakikisha linakuwa la kisasa zaidi .
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa ,Juma Homera Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ,Dkt. Rashid Chua chua amesema kuwa kwa maslai mapana ya Taifa watasimamia kuona miradi yote inakamilika kwa wakati.
Dkt. Chua Chua amesema kuwa ifikapo April mwaka huu 30,mwaka huu miradi yote ya ujenzi na ukarabati ya miundombinu katika hosptali za Wilaya, Vituo vya afya na Zahanati vinakamilika kwa wakati.
Amesema kuwa miradi yote iliyobaki itakamilika kwa wakati kama walivyopanga.
More Stories
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari