Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Songea
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Innocent Bashungwa amefungua mkutano wa Sita wa Mkuu wa Majeshi na Makamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Unaofanyika Mjini Songea.
Akifungua mkutano huo leo Januari 23,2023 mjini Songea , Waziri Bashungwa amesema Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeendelea kuwa na Mahusiano mazuri na Majeshi Mengine sambamba na Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini.
Kwa mujibu wa Waziri huyo , Serikali imeendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kuliboresha Jeshi kwa watu, Zana na Vifaa.
Katika hatua nyingine Waziri Bashungwa amebainisha kuwa mwenendo wa Jeshi ni mzuri na linaendelea kufanya vizuri katika operesheni za Umoja wa Mataifa.
“Mwenendo wa Jeshi la wananchi Tanzania chini ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda ni mzuri ,taswira ya Jeshi mbele ya jamii ni chanya ,mahusiano ya majeshi yetu na mahusiano ya majeshi ya nchi jirani kwenye mazoezi ya pamoja kikanda na majukumu ya ulinzi wa amani ni mazuri na nidhamu, utii ,uhodari ,ujasiri na uaminifu kwa maafisa na skari ni wa hali ya juu .”amesema na kuongeza kuwa
“Mafanikio hayo yamewezekana kwa sababu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ,Makamanda wote ndiyo wasimamizi wakuu wa majeshi yetu ambao ni usimamizi wenye weledi.”amesisitiza Waziri Bashungwa
Ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuyawezesha majeshi hapa nchini na hivyo kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Aidha amewaasa Wakuu wa Vikosi, shule na vyuo wasimamie vyema maeneo wanayopewa kwa maana ya kuyalinda .
“Nazungumzia migogoro ya ardhi na mkakati wa Wizara na Ngome kufanya upimaji na maeneo yote ya Jeshi lazima yapate haki miliki ili kuwa na nguvu ya kisheria ‘legal force’ dhidi ya uvamizi ambao unaendelea maeneo mbalimbali ya viosi vyetu.”amaesema
Naye, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob Mkunda ameshukuru serikali za awamu zote nchini kwa kuliwezesha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kutekeleza majukumu yake.
Aidha, Jenerali Mkunda ameahidi kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufuata sheria, na kuhakikisha kuwa Jeshi lipo timamu na lipo tayari kukabidhiwa majukumu litakayopangiwa na serikali.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini