Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa(Mb) amesema Jeshi la Kujenga Taifa litashirikiana na Wizara za Kisekta za Uzalishaji na taasisi zake, kubuni na kupanua wigo wa Kazi ili kutengeneza ajira kwa Vijana wanaomaliza Mafunzo ya kujitolea katika Jeshi la kujenga Taifa.
Bashungwa amesema hayo leo tarehe 06 Februari 2023 Bungeni jijini Dodoma wakati alitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizoibuliwa na Wabunge wakati wa kujadili taarifa ya Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
Amesema Serikali itapanua wigo ili kuwawezesha vijana hao wanapata fursa za ajira ikiwemo katika Masuala ya kilimo kamÄ… skimu za Umwagiliaji, Kuzalisha Mbegu na mazao ya chakula na katika shughuli nyingine.
Bashungwa amesema Jeshi la Kujenga Taifa litajikita kutoa mafunzo sawa na mitaala inayofundishwa katika vyuo vya ufundi stadi ili kijana anayehitimu Mafunzo ya JKT anakuwa na ujuzi sawa na Mhitimu wa vyuo vya VETA.
Aidha, amefafanua kuwa Serikali imeweka jitiahada ya kuhakikisha vijana wanaomaliza mafunzo ya JKT wanapata ajira kwenye vyombo vya ulinzi na Usalama ambapo takwimu zinaonesha asilima 45 ya vijana waliojiunga na JKT katika mwaka 2018, 2019 na 2020 wamepata ajira kwenye vyombo vya ulinzi na Usalama.
Kadhalika, Basungwa amesema Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa itafanyia kazi mapendekezo na maoni mbalimbali yaliyotolewa na Wabunge ikiwa ni pamoja na kuweka alama za mipaka na Barabara za ulinzi.
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano