Na Hamis Miraji, Timesmajira
Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), limemfutia usajili pamoja na cheti chake cha sanaa msanii wa muziki wa bongo fleva Godfrey Tumaini maarufu ‘DuduBaya’ , kutokana na kutofuata maadili katika tanga hiyo.
Msanii huyo amefutiwa cheti chake cha usajili chenye namba BST.2184,ambapo kuanzia sasa haruhusiwi kujishughulisha na sanaa hapa nchini.
Hatua hiyo imekuja, baada ya msanii huyo kutumia lugha ya matusi kwa wadau wa sanaa kupitia kwenye akaunti yake ya instagram, huku akitambua kuwa kufanya hivyo ni kosa kutokana na kanuni za BASATA.
Kwa mujibu wa barua ya BASATA iliyosainiwa na katibu mtendaji wa baraza hilo Godfrey Mngereza Dudubaya amefutiwa usajili huo, kuanzia April 16 mwaka huu.
More Stories
Wassira:Waliopora ardhi za vijiji warudishe kwa wananchi
Rais Samia apongezwa kwa miongozo madhubuti ya ukusanyaji wa kodi
Mwenda:Siku ya shukrani kwa mlipakodi ni maalum kwaajili ya kuwatambua,kuwashukuru