Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Wasanii wa Tanzania wametakiwa kuunga mkono kampeni ya SENSABIKA iliyozinduliwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo (Mb) Mohamed Mchengerwa kwa kubuni nyimbo na mabango mbalimbali ya sanaa za ufundi ili kuhamasisha watanzania kujitokeza kuhesabiwa katika sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2022.
Hayo ameyasema leo Katibu Mtendaji wa BASATA Dkt. Kedmon Mapana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam akifafanua suala la Mdundo wa Taifa na Tamasha la Sensabika ambayo yataongeza uchumi wa watanzania na wasanii kwa ujumla.
Dkt. Mapana amesema yeye kama mmoja wa wanakamati wa kutafuta mdundo wa Taifa atahakikisha Mdundo unapatikana na watanzania wanakua na furaha wakati matukio mbalimbali ya sanaa nchini yanafanyika ipasavyo;
“Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) tutahakikisha watanzania wanakua na furaha na faraja wakati kwa kuhakikisha matukio ya sanaa yanafanyika kwa weledi nchini, Matamasha mbalimbali yatakuwa yanafanyika ikiwemo ya ngoma, muziki wa dansi, bongo Fleva, Taarabu ili kuhakikisha utajiri wa sanaa tuliojaliwa Tanzania tunautumia ipasavyo”
Aidha Dkt. Mapana amesema watakua wanaibua matukio makubwa mbalimbali kama vile matukio ya ufundi kwa kuhakikisha maonyesho mbalimbali yanakua yanaendelea nchini Tanzania.
Pia Dkt. Mapana amesema Dhana ya serikali inatafuta utambulisho kwenye muziki namna gani wataalamu wa muziki wakiwemo Dj, Producer, waimbaji, wanaweza wakakaa pamoja na wakafanya tafiti na kutoa mawazo ya pamoja ili kuweza kutengeneza kitu ambacho kitaleta utambulisho wa Taifa.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini