Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online, Musoma
BARABARA mbalimbali za jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, zimejengwa na nyingine kukarabatiwa katika mwaka wa fedha wa 2020/2021, ambao uliishia Juni 30 mwaka huu.
Nyingine zaidi zinatarajiwa kujengwa na kukarabatiwa katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 kwa Sh. bilioni 2.85 ili kurahisha usafiri na usafirishaji wa mazao ya wakulima kutoka vijiji mbalimbali vya jimbo hilo.
Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA), Wilaya ya Musoma, Mhandisi Abbas Hussein amezitaja baadhi ya barabara zilizokamilika katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 kuwa ni ya kijiji cha Bukima, Bulinga hadi Bwasi na kijiji cha Nyegugu, Rusoli hadi Makojo.
“Nyingine ni ya kutoka katika kijiji cha Butata, Kastamu, Kastamu hadi Kumsoma na kutoka kijiji cha Busungu, Bulinga hadi Bujanga, ujenzi na ukarabati wake ulikamilika Juni 30 mwaka huu,” alisema Mhandisi Hussein.
Amesema, jumla ya Sh. milioni 90.5 zimetuka katika ujenzi na ukarabati wa barabara hizo na kwamba, katika mwaka wa fedha wa 2021/2022, zitajengwa na ukarabati wa barabara nyingi zaidi.
“Musoma Vijijini kuna vijiji 68, miongoni mwa barabara hizo ni ya kijiji cha Masinono hadi Kinyang’erere, kijiji cha Mkirira hadi Hospitali ya Mkoa wa Mara iliopo Kwanga, kutoka Mkirira, Nyegina hadi Etaro,”amesema.
Mhandisi hiyo ameendelea kutaja barabara nyinginza zaidi kuwa ni ya kutoka kijiji cha Nyaminya, Kataryo hadi Kyawazaru, Maneke, Mayani hadi Kyawazaru, Mugango, Bwai hadi Kwikuba.
“Zipo pia barabara za vijiji vya Bwai Kwiturutu hadi Bwai Kumsoma, Chirorwe hadi Wanyere, Saragana, Nyambono hadi Chumwi, Mabuimerafuru hadi Murangi na Bwasi hadi Kome,” amesema.
Mbali na hizo, meneja huyo aliendelea kutaja barabara nyingine ambazo zitakajengwa na kukarabatiwa kuwa ni za vijiji vya Chitare, Kurugee hadi Buraga, Bukumio hadi Burungu na Busekera hadi Burungu.
More Stories
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi