Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
SERIKALI ya Tanzania inatarajia kuanza ujenzi wa bandari ya uvuvi Kilwa mkoani Lindi, kwa lengo kuchochea maendeleo ya uchumi wa Buluu katila Taifa letu.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam leo na mkurugenzi Msaidizi wa utafiti na mafunzo ya uvuvi kutoka wizara ya mifugo na Uvuvi Dkt Erastusi Mosha wakati akifungua kikao cha wadau wa uvuvi kilicholenga kujadili taarifa ya upembuzi yakinifu ya ujenzi wa bandari hiyo.
Dkt. Mosha amesema uwekezaji huo utakuwa na manufaa kwa wakazi wa maneo hayo na taifa kwa ujumla pamoja na nchi jirani na Tanzania ambazo hazina Bandari ya Uvuvi.
“Kwa kipindi kirefu tangu Uhuru Tanzania atujawahi kuwa na bandari ya uvuvi kutokuwepo kwa bandari hiyo kumesababisha meli ambazo zimekuwa zikivua katika ukanda wa uchumi wa bahari kutoweza kuja kutua mizingo yao katika bandari yetu”alisema Dkt Mosha
Amesema mradi huo wa Ujenzi utajengwa kwa muda wa miaka mitatu kuanzia mwaka huu ambapo utasaidia meli zote za nje kupata mahitaji yao kutoka nchini jambo litasaidia uchumi kuongezeka zaidi.
Alibainisha kuwa Julai 2 mwaka 2018 serikali iliingia mkataba na kampuni ya Itali kwa ajili ya kuandika upebuzi yakijifu ili kuona ni eneo gani mradi huo utaweza kujengwa
“Maeneo yaliopitiwa ni mengi serikali iliamua bandari ya uvuvi itajengwa katika eneo la kilwa ambapo baada ya kujengwa meli zote ambazo zimepewa leseni zitaweza kutua mizingo katika bandari yetu”alisisitiza
Awali Mkurugenzi msaidizi uendelezaji wa rasilimali za uvuvi, aliyemwakililisha mkurugenzi wa uvuvi Merisia Mparazo alisa mradi huo ni wa kimkakati ambao umelenga kulisaidia taifa kutumia rasilimali zake.
“Mradi huu utaisaidia nchi kuvuna rasilimali zilizopo katika bahari ,kutegeneza ajira na kuleta tija kwa nchi kwa ujumla sambamba na uwepo wa viwanda vya kuchakata samaki”alisema
Merisia amesema katika hatua za awali wameamua kuwashirikisha wadau wote wa masuala ya uvuvi ili kuleta tija zaidi katika utekelezaji wa mradi huo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa katibu Tawala wa mkoa wa Lindi ambaye ni katibu Tawala msaidizi Ramadhani Hatibu amesema Mkoa huo umeupokea vizuri mradi huo kutokana na kuwa na tija kwa taifa na jamii kwa ujumla.
Amesema kutokana na mradi huo kutasaidia kuvua samaki wenye ujazo mkubwa ambao utasaidia Pato kwa taifa .
Khalfan Shabani Muhogo ambaye ni mdau wa Uvuvi amesema kuwa Ujenzi wa bandari hiyo ya Uvuvi utaleta maendeleo makubwa katika sekta ya uvuvi .
Aidha aliiomba serikali kuwakaribisha wawekezaji kwa ajili ya ujenzi wa karakana ya meli baada ya ujenzi wa bandari hiyo kukamilika.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini