January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Balozi Siwa afungua mkutano wa 50 Baraza kuu la wafanyakazi NSSF

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Balozi Ali Idi Siwa, amefungua Mkutano wa 50 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF.

Katika Mkutano huo, Balozi Siwa alisisitiza uboreshaji wa huduma bora kwa wanachama, kuendelea kuwajengea uwezo wafanyakazi, kuongeza kasi ya ukuaji wa Mfuko kwa kuifikia sekta binafsi na sekta isiyo rasmi na kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utendaji kazi.

Lengo la mkutano huo ni kupitia Mpango wa mwaka ujao wa fedha na bajeti kwa mwaka 2023/2024, ikiwa ni ushirikishwaji wa wafanyakazi katika maamuzi ya kiutendaji. Ufunguzi wa mkutano huo umefanyika tarehe 18 Aprili 2023 katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Balozi Ali Idi Siwa, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF.
Mkutano huo ulifanyika Aprili 18, 2023 katika ukumbi wa AICC, jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, akitoa maelezo ya awali kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi uliofanyika jijini Arusha. Mkutano huo ulifunguliwa na Balozi mstaafu Ali Idi Siwa ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala wa NSSF, Ekwabi Mujungu, alipata fursa ya kutoa salamu katika mkutano wa 50 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi la NSSF. Mujungu amesisitiza kuendelea kusimamia maslahi ya wafanyakazi na pia alitoa wito kwa wafanyakazi kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma.
Katibu Msaidizi wa Sekta ya Taasisi za Fedha TUICO, Victor Leonard Kom akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wajumbe wa Mkutano w Baraza kuu la Wafanyakazi wa NSSF. Mabaraza ya wafanyakazi yapo kisheria kwa madhumuni ya kutoa ushauri na kusimamia haki na ustawi sehemu za kazi.
Wajumbe wa mkutano wa 50 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakifuatilia kwa makini mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa AICC, jijini Arusha.