June 7, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Balozi Nchimbi ashiriki mazishi ya Mzee Songambele

*Songambele ni mmoja wa wapigania Uhuru wa Tanganyika

*Mmoja wa waasisi wa TANU,CCM

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi hivi punde amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Songea, mkoani Ruvuma na kupokelewa na viongozi wa chama na Serikali mkoani humo, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed na Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Mohamed Ali Khalfan, leo Juni 2, 2025.

Balozi Nchimbi amewasili mjini Songea, kwa ajili ya kushiriki mazishi ya mwanasiasa mkongwe na mmoja wa wapigania uhuru wa Tanganyika, na waasisi wa Chama cha TANU na CCM, Alhaj Mustafa Songambele, aliyefariki usiku wa kuamkia Juni 1, 2025 jijini Dar es Salaam na kutarajiwa kuzikwa leo mkono humo.