January 27, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Balozi Kombo :Maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu nishati yakamilika, Marais 25 kuhudhuria

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amesema Maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati ujulikanao kama Mission 300 yamekamilika, ambapo  zaidi ya marais 25, Mawaziri Wakuu na Manaibu Mawaziri wakuu, Mawaziri wa Fedha na Nishati 60 wa Afrika watashiriki.

Mkutano huo unaotarajia kufanyika Januari 27 na 28 Jijini Dar es Salaam, utawakutanisha Viongozi hao Wakuu wa Nchi lengo likiwa ni kujadili namna ya kutumia fursa ya ushawishi kwa wadau wa maendeleo kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya nishati jadidifu, ambayo ni rafiki kwa mazingira

Aidha, viongozi wengine wa kimataifa watashuhudia wakuu wa nchi za Afrika wakikubaliana kusaini Mpango Mahususi wa Nishati wa Afrika, awamu ya kwanza utakaozishirikisha nchi 14 ambazo ni pamoja na Tanzania, Malawi, Chad, Nigeria, Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Niger, Liberia, Msumbiji, Madagascar, Zambia, Mali, Ivory Coast na Mauritania.

“Baada ya Mkutano huo, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pia anatarajia kuwa na mazungumzo na wakuu hao wa nchi kuzungumzia masuala ya ushirikiano na nafasi ya Tanzania katika kushirikiana na nchi hizo, nchi ambazo wakuu wa nchi wamethibitisha kuwepo ni pamoja na Algeria, Visiwa vya Comoro, Malawi, Zambia, Sierra Leone, Liberia, Somalia, Lesotho, Botswana, Guinea Bissau, Kenya, Burundi, Mauritania, Congo Brazzaville, Madagascar, DRC Congo, Libya, Khartoum Sudan, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Djibout, Togo na Rais wa Gabon” amesema Balozi Kombo.

Amesema viongozi wengine watakaohudhuria ni Makamu wa Rais wa Gambia, Makamu wa Rais wa Benin, Waziri Mkuu wa Côte d’Ivoire, Waziri Mkuu wa Uganda, Waziri Mkuu wa Visiwa vya Sao Thomé, Waziri Mkuu wa Equatorial Guinea, Naibu Waziri Mkuu wa Ufalme wa Eswatini, Naibu Waziri Mkuu wa Namibia.

“Na pia tunatarajia kuwa na Mawaziri mbalimbali kwani kuna nchi ambazo zitawakilishwa na Mawaziri na Manaibu Waziri wakuu, Afrika Kusini itawakilishwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa nchi hiyo atahudhuria mkutano huo,Waziri wa Nishati, Viwanda na Madini wa Tunisia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Falme za Kiarabu, Waziri wa Nishati kutoka Rwanda, Waziri wa Nishati Morocco, Waziri wa Nishari Zimbabwe, na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa’ Amesema Balozi Kombo na kuongeza kuwa wengine watakaoshiriki ni Rais kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt. Akinwumi Adesina na Rais wa Benki ya Dunia Bw. Ajay Banga.

“Nia ya mkutano huu ni kuwawashia taa, umeme, mwangaza pamoja na mapishi ya kutumia nishati safi milioni 300 Barani Afrika na Mhe. Rais wetu ndio kinara, ukijiuliza watanzania tupo miliuoni 62 tu,lakini rais wetu anakwenda kutuwashia umeme watu milioni 300 mara tano zaidi ya idadi yetu kwa kushirikiana na wenzake,kwa hiyo kutakuwa na marais 12 ambao watakuwa na majukwaa ya pembeni ambao kwa pamoja wakiongozwa na rais wetu pamoja na Benki ya Dunia (WB) na Benki ya Afrika (AfDB) watapeleka nishati safi ili kuwakinga wananchi kwa maradhi ya kifua kwa kupika na kuni” amesema Balozi Kombo.

Awali akizungumza na vyombo vya Habari, Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeshughulikia masuala ya nishati na mabadiliko ya hali ya hewa, Dk Kevin Kariuki, alisema mkutano huo ni muhimu kwani utakutanisha wakuu wa nchi na viongozi wengine ambao baada ya kujadiliana, watasaini Azimio la Dar es Salaam linaloweka makubaliano yaliyofikiwa kutekelezwa kuhusu mkutano huo muhimu ambapo watashuhudia viongozi hao wakikubaliana na kuingia mkataba wa kuwezesha lengo la kusambaza umeme kwa watu milioni 300 kabla ya 2030 kufikiwa.

Amesema Benki ya Dunia na AfDB, Aprili mwaka jana walikubaliana kuwa haiwezekani wananchi wa Afrika wakaendelea .