December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Balozi Dkt. Chana aitaka mikoa,
wilaya kuipa kipaumbele michezo

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Balozi Dkt. Pindi Chana, ameshiriki kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Njombe kilichohudhuriwa na viongozi na watendaji wa Idara na Taasisi mbalimbali za mkoa huo.

Balozi Dkt. Chana ametumia fursa hiyo kusisitiza Mikoa na Halmashauri zote nchini zitenge fedha za kukarabati na kujenga miundombinu kwa ajili ya shughuli za Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Aidha, ametoa wito kwa viongozi wa Halmashauri na mikoa kote nchini waendelee kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendeleza shughuli za Utamaduni, Sanaa na Michezo kutokana na umuhimu wake katika kukuza na kutoa fursa za ajira kwa vijana ambao ni wengi hapa nchini.