December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BAKWATA,yafungua msikiti mpya wa Al-Ghazal

Na Daud Magesa, Timesmajira Online, Mwanza

Baada ya msikiti wa zamani kuvunjwa kwa ajili ya kupisha ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Hasani Kabeke,amefungua Msikiti wa Al-Ghazal, uliopo Kata ya Mahina wilayani Nyamagana.

Akizungumza katika hafla ya kufungua msikiti huo wa Al-Ghazal,Sheikh Kabeke amesema,waumini wa dini ya kiislamu waache kusikiliza maneno ya ovyo, yenye kuwatisha tamaa katika kuchangia miradi na kujieletea maendeleo yao.

“Tukio hili ni la kihistoria la kufungua msikiti huu wa Al-Ghazal Mahina,yalisemwa mengi kuhusu fedha za ujenzi wa msikiti huu .Lakini leo msikiti umefunguliwa wa kisasa baada ya kuvunjwa wa zamani kupisha mradi wa SGR,”amesema Sheikh Kabeke bila kufafanua.

Pia amewataka wasaidizi wake,waendelee na mwendo wa kuziba masikio kama chura kiziwi iii waweze kuweletea waislamu maendeleo na Mwanza kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Sheikh huyo wa Mkoa wa

Katika hatua nyingine Sheikh Kabeke ameongoza dua ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan,Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania na wote waliosimama imara kusimimia fedha za fidia zilizotolewa na serikali na kuwezesha kupatikana msikiti huo wa Kisasa wa Al-Ghazal,yenye madrasa nzuri ya kisasa na ofisi nzuri.