January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Baba asakwa kwa kumuua mtoto wake

Na Judith Ferdinand,TimesMajira Online, Mwanza

JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linamsaka baba mzazi, Adam Athuman (30-40) kwa tuhuma za za kumuua mtoto wake huko katika Kata ya Buswelu Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza.

Tukio hilo lilitokea Novemba 22, 2020 majira ya saa 5:30 huko Kata ya Buswelu wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Akizungumza mkoani hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Muliro Jumanne amesema, marehemu huyo ambaye jina lake ni Athuman Adam mwenye umri wa miaka 10 aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Nyamadoke Kata ya Buswelu Wilaya ya Ilemela,aliuawa kwa kile kilichodaiwa kushambuliwa na fimbo sehemu za mwili wake.