Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
Matajiri wa Jiji, Azam FC inemanikiwa kumnasa kiungo mkabaji wa kimataifa wa Rwanda, Ally Niyonzima aliyesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo.
Niyonzima aliyekuwa akicheza Rayon Sports ya Rwanda, usajili wake ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba.
Niyonzima amesajiliwa na Azam akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kuripotiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Kabla ya Azam kumnasa Niyonzima, kiungo huyo alikuwa kujiunga na klabu ya Yanga na kudaiwa kuwa tayari ameshamalizana na viongozi na alichokuwa akisubiri ni kuweka saini tu mkataba wake mpya.
Niyonzima, ambaye yupo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Azam FC kwa ajili ya msimu ujao.
Usajili wa kwanza ulikuwa ni wa kiungo Awesu Awesu, kwa usajili huru akitokea Kagera Sugar.
More Stories
Watumishi wa Fahari wafanya Bonanza
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship