January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Azaki zaomba kitofautishwa na taasisi binafsi

Na Queen Lema,Timesmajira Online, Arusha

Asasi za kiraia(Azaki)zimeomba serikali kuweza kuwatofautisha na asasi binafsi kwa kuwa mpaka sasa bado kuna mwingiliano mkubwa hasa katika masuala ya wafadhili.

Hayo yameelezwa na Rais wa taasisi ya Foundation For Civil Society Dkt. Stigmata Tenga wakati akifunga mkutano wa Azaki uliokuwa unafanyika jijini Arusha.

Ambapo amesema kuwa lengo la asasi zisizo za Kiserakali pamoja na Azaki zote zipo Tanzania lakini malengo ni tofauti,

Amefafanua kuwa kwa kushindwa kutofautisha asasi hizo imepelekea baadhi ya wafadhili kupeleka fedha Kwa asasi hizo huku Azaki kushindwa kupata haki zao.

“Tunaomba tusaidiwe kwa kuwa kuna agenda nyingi ambazo tumeshindwa kuzikamata, na sauti yetu ni moja tu,”.

Katika hatua nyingine amesema kuwa Azaki imejipanga katika kuhakikisha kuwa wanaendelea kuboresha mambo yao ikiwa ni pamoja na kuwa na matamasha kila mwaka Ili waweze kujifunza.

“Mwakani tutasogeza matamasha ambapo mabadiliko yote yanalenga kuwafanya washiriki waweze kufurahia Lakini pia kujifunza na kuongeza ufanisi zaidi”