Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
BAADA ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Azam, aliyekuwa kiungo wa Kagera Sugar, Awesu Awesu ameahidi kuifanyia makubwa hiyo.
Awesu anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Azam FC kwenye dirisha kubwa la usajili kwa ajili ya msimu ujao, ukiwa ni usajili huru baada ya kumaliza mkataba wake Kagera Sugar.
Kiungo huyo ambaye amewahi kulelewa kwenye kituo cha Azam Academy miaka miwili 2014-2015, amesaini mkataba huo leo Alhamisi jioni mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’.
Azam imemsajili nyota huyo baada ya kuonesha kiwango kizuri kwa misimu miwili mfululizo akiwa na Singida United na msimu huu Kagera Sugar, huku katika mashindano yote msimu huu akifanikiwa kufunga goli saba.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo mpya, Awesu amesema kuwa, kikubwa anachowaahidi mashabiki wa klabu hiyo ni kuonesha makubwa zaidi kwani alitamani siku moja kurudi kuja kuyafanya ndani ya klabu hiyo.
“Niliondoka Azam nikiwa mdogo na sasa nimerudi hivyo nitafanya mambo makubwa na nimerudi kwa sababu hiyo kwani nilitegemea kufanya hivyo baadaye kwani nilitamani kuja kucheza tena Azam na sasa ana furaha kubwa kurudi nyumbani, ” amesema Awesu.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM