March 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

AUWSA yazipatia maji kaya 6000 za kipato cha chini

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA)kwa kushirikiana na Mamlaka za maji Uholanzi (VEI) tunatekeleza programu ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa kaya za kipato cha chini ambapo jumla ya kaya 6000 zimenufaika.

Hayo yamesemwa jijini hapa leo Machi 14,2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa AUWSA Mhandisi Justine Rujomba,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Mamlaka hiyo ofisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita,ambapo amesema Programu hiyo ni endelevu kwa sasa.

Mha.Rujomba amesema hayo ni katika kufanikisha lengo namba moja na lengo namba sita la maendeleo endelevu Tanzania (SDG 6) “kuongeza kipato cha watu waishio kwenye umaskini na kuhakikisha wanapata huduma za msingi na kumlinda kila mtu kuepukana na majanga Pamoja na kuhakikisha  upatikanaji wa majisafi na salama kwa kwa watu wote.

Aidha Mha.Rujomba amesema kuwa katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kuboresha huduma kwa  kuongeza Masaa ya huduma ya Maji
Masaa ya upatikanaji wa huduma ya maji yameongezeka kutoka saa 16 (2020/21) hadi saa 22 mwaka 2024/25.

Huku idadi ya wateja waliounganishwa na huduma za maji imeongezeka kutoka 71,183 (Juni 2021) hadi 134,000 hadi kwa sasa.

Vilevile amesema utekelezaji wa Miradi ya maji kupitia ufadhili wa Serikali ya Tanzania Pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), AUWSA imekamilisha mradi mkubwa wa maji kwa lengo la kuboresha hali ya upatikanaji wa majisafi na kuboresha huduma ya uondoaji wa majitaka katika jiji la Arusha ili kuboresha afya na hali ya maisha ya wakazi wa Jiji kwa ujumla wake. 

“Mradi huu umegharimu Shilingi za Kitanzania Bilioni 520,”amesema Mha.Rujomba.

Pamoja na hayo Mha.Rujomba amezungumzia
Vipaumbele vya Bajeti 2024/252025/2026
Katika mwaka wa fedha 2024/252025/2026, AUWSA inalenga kupunguza maji yanayopotea na kuongeza mapato,kusogeza huduma na kuunganisha wateja na Kuboresha huduma kwa mteja

Vilevile ametaja shughuli zitakazotekelezwa kuimarisha huduma
katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/252025/2026,amesema AUWSA imepanga kutekeleza shughuli mbalimbali zitakazogharimu  TZS bilioni 11.874.2, ili kuimarisha huduma.

“Shughuli hizo ni pamoja na kujenga mtandao mpya wa maji safi wa km 215.96
,Kuunganisha wateja wapya 13,9⁶93,kuongeza mtandao wa majitaka kwa km 10,kuunganisha wateja 4,200 kwenye huduma ya majitaka na uboresha mtandao chakavu wa maji safi kwa km 64,”amesema.